BVR YAGEUKA MATESO KWA WATANZANIA SOMA HAPO KUJUA
![]() |
| Waandikishaji wakiwa kwenye foleni wa BVR |
UANDIKISHAJI wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura kwa mfumo wa kielektroniki (BVR), umechukua sura mpya
kutokana na baadhi ya watu kuwauzia nafasi wengine katika vituo vya
kujiandikishia. Anaandika Ferdinand Shayo … (endelea).
‘Wafanyabiashara’ hayo wamekuwa wakiwahi nafsi mapema na kisha kuziuza kwa wale ambao wanashindwa kuwahi hasa pale foleni inapokuwa ndefu na hata wengine kulazimika kulala vituoni.
Wananchi wa Kata ya Sinoni jijini hapa
Hussein Issa na Swalehe Ramadhani wameeleza kuwepo kwa baadhi ya vijana
ambao tayari wameandikishwa lakini hufika tena kituoni hapo mapema na
kushika nafasi za mbele na baadaye huwauzia watu wengine, mchezo huu
umekithiri katika vituo vingi.
Issa amesema kuwa, nafasi moja huuzwa kati ya Sh. 10,000 hadi 15,000 kwa mtu mmoja na kwamba, hugombaniwa na watu wengi.
“Watu wamegeuza BVR kama biashara,
wanashika nafasi na kuwauzia watu jambo ambalo linakwamisha zoezi. Watu
wengi wasiokuwa na kitu cha kutoa wanakaa kwenye foleni kwa muda mrefu
bila kuhudumiwa,” amesema Issa.
Polpodia Massawe ambaye ni Mkazi wa Esso
amelalamikia tabia mfumo huo wa BVR kuwa bado haujaweza kukidhi idadi
kubwa ya watu kwani imemlazimu kuacha shughuli za kujiingizia kipato na
kupanga foleni kwa muda wa siku 4 bila mafanikio.
Ameasema kuwa, watu wengine wamekuwa
wakikesha na kulala vituoni hapo ili kuwahi nafasi ambapo ameitaka
serikali iongeze nguvu hasa kwenye vituo vya mijini vyenye idadi kubwa
ya watu.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Filex
Ntibenda aliyetembelea kituo hicho, amekaripia vikali tabia ya watu
kuuza nafasi maarufu kama ‘ploti’ kwani ni kinyume cha utaratibu.
Ntibenda pia amewataka wanasiasa kutoingilia uandikishaji ambapo amehamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi.
kwa hisani ya Mwanahalisi oline

1 comment
Zoezi zima la uandikishaji halijaenda vizuri kama tulivyotazamia ama kwa makusudi fulani au kwa uzembe. Bahati mbaya serikali haina hata muda wa kucalculate muda wa wananchi wake wanaoupoteza kwa kupanga mistari hadi siku 4. Huku kwetu nimeshuhudia jinsi ambavyo waandikishaji wamepewa uhuru mkubwa wa kuharibu zoezi hili kwa makusudi mfano: wanaita ndugu, jamaa na rafiki zao bila kufuata foleni na kusababisha vurugu zisizo za lazima. Pia kioja kilitokea katika kituo kimoja nilichokuwa naandikishwa ilipobainika kuwa muandikishaji mmoja alipewa kibarua hicho huku akiwa hafahamu kusoma wala kuandika.
Post a Comment