BENKI KUU YAIKINGIA KIFUA TENA SARAFU YA SHILINGI 500,SOMA HAPO KUJUA

Benki
Kuu imekanusha vikali kwamba sarafu ya shilingi 500 ina madini ndani yake hivyo
ni mali inayoweza kutumika kutengenezea vito, kufuatia uvumi potovu ulioenea
kila pembe ambao unawafanya wananchi wengine wanunue sarafu hiyo kwa bei mara
tano hadi kumi y thamani yake.
Akiongea na Globu ya Jamii jijini Dar es salaam leo, Meneja wa vituo vya Utunzaji wa Benki Kuu Bw. Abdul Dollah, amesema kwamba uvumi huo si kweli na kwamba katika sarafu ya shilingi 500 kuna madini machache mno ya nickel ambayo hayafai hata chembe kutengenezea vidani.
Amesema sio kweli kwamb sarafu za shilingi 500 hazipo katika mzunguko kutokana na kuhodhiwa na hao wenye kuvumisha na wanaotaka faida ya haraka haraka, na kwamba zinapatikana kwa wingi katika vituo vyake vyote.
Amesema huenda wananchi wanachanganya sarafu hiyo ya 500 na sarafu maalumu iliyotolewa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ambayo alikiri kwamba ina madini na thamani yake ni shilingi 50,000/-
Video ya mahojiano na Bw. Dollah inaandaliwa
na itarushwa hewani si muda mrefu ujao. Tuvute subira...

No comments
Post a Comment