ZOEZI LA KUANDIKISHA WAPIGA KURA YAKUBWA NA KASORO NYINGI:TACCEO
Zoezi la undikishaji
kwa wapiga kura kwa mfumo wa Kielektroni linaonekana kuingia doa
kufuatia mapunguvu mengi kuibuka huku hatua za haraka kuchukuliwa zikionekana
kuzorota.
Hayo yamesemwa leo jijini Dare s salaam na mwenyekiti wa
mtandao huo Ms MARTINA KABISAMA wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari
kuhusu zoezi la uandikishwaji wa wapiga kura kwa mfumo wa kielektronic BVR unaoendelea
huko mikoani
Ametaja changamoto ambazo zinalikabili zoezi hilo kwa sasa
kuwa ni pamoja na idadi ndogo wa wanancchi wanaojitokeza katika vituo vya
kujiandikisha na baadhi ya raia kusajiriwa bila kuchukuliwa alama za vidole.
Kabisama amesema Katika uangalizi wao katika mikoa ya Njombe,Lindi,Mtwara, na Ruvuma wamebaini
ukiukwaji mkubwa wa sheria,na kanuni za uchaguzi pamoja na maelekezo ya tume ya
taifa ya uchaguzi huku akisema kuwa endapo mapungufu hayo hayatafanyiwa kazi
kwa haraka iwezekanavyo itapelekea
wananchi kupoteza haki yao ya msingi ya kujiandikisha na kushiriki katika
uchaguzi kwa mujibu wa sheria.
Akitaja baadhi za changamoto za ukiukwaji wa sheria
zilizotokea katika mikoa ambayo zoezi hilo linaendelea Ms KABISAMA amesema kuwa,kutokutolewa kwa
elimu ya mpiga kura vijijini, wananchi kuandikishwa bila alama za vidole,
uandikishwaji kufanya hadi saa sita usiku,pamoja na vituo vya uandikishwaji
kuwekwa katika nyumba za ibada,hospitali na kwenye mabanda ya mama lishe ni
moja kati ya mambo ambayo yamekuwa yakijitokeza katika zoezi hilo.
Nyingine ni uandikishwaji kushindwa kufanyika kwa wakati
kutokana na kukosekana kwa mashine za kuandikishwa na kuishiwa kwa
chaji,wananchi wengi kuachwa kuandikishwa kutokana na kumalizika kwa siku saba
zilizopangwa kwa ajili ya maeneo hayo, nazo zimekuwa sababu ambazo amezitaja
kama zinaweza kukwamisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.
Aidha amesema kuwa kutokana na kasoro hizo zilizojitokeza (TACCEO)
wamaitaka tume ya Taifa ya uchaguzi ihakikishe kuwa inarekebisha kasoro hizo
ikiwa ni pamoja na kurudia maeneo ambayo wananchi walikosa haki hiyo ya
kujiandikisha kwani ni haki yao ya msingi,huku akiitaka tume hiyo kuruhusu
asasi za kiraia kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ili kuweza kuhamasisha
kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo.
Mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi Tanzania
TACCEO unaoratibiwa na kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC umekuwa
ukishiriki uangalizi wa zoezi la uandikishwaji wapiga kura kwa kutumia mfumo
mpya wa kielektronic BVR ulioanza rasmi tarehe 23,mwezi wa pili 2015 katika
halmashauri ya mji wa makambako
No comments
Post a Comment