ALIYERUHUSU KUIBIWA MABILIONI YA ESCROW ASAFISHWA SOMA HAPA KUJUA

BALOZI Ombeni Sefue- Katibu Mkuu Kiongozi,
amesema uchunguzi uliofanywa dhidi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini, Eliachim Maswi, haukumkuta na hatia yoyote katika kashfa ya ukwapuaji
fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT)… Anaadika Mwandishi Wetu … (endelea).
Balozi Sefue alimsimamisha kazi Maswi
kwa muda kuanzia Desemba 23, 2014, kwa kutumia madaraka aliyonayo kama Mamlaka
ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo makatibu wakuu
ili kupisha uchunguzi dhidi yake.
Hata hivyo,
akizungumza na waandishi wa habari leo Ikulu jiji Dar es Salaam, Balozi Sefue,
amesema uchunguzi umekamilika na Maswi amebainika kutotenda kosa lolote ya
kinidhamu katika sakata hilo.
Amesema kuwa
kutokana na uchunguzi huo, mamlaka ya uteuzi wake (Rais) ambayo ilikuwa
imemsimamisha, imeachiwa kuamua hatua za kuchukua dhidi yake ikiwa ni pamoja na
kumresha kazini au kumpangia majukumu mengine.
Wakati wa kusimamishwa
kwake, Balozi Sefue alisema kuwa amechukua hatua hiyo “Kwa mujibu wa Kifungu
4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002 (kama
ilivyorekebishwa)”ambapo “Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa
Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.
Badala yake, Balozi
Sefue alisema kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi
Ngosi C. Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini
hadi uchunguzi dhidi ya Maswi utakapokamilika.
Wakati Maswi
akisafishwa na Ikulu katika kashfa hiyo, tayari aliyekuwa waziri wake, Prof.
Sospeter Muhongo amejiuzulu tangu 24 Januari 2015, kwa kile alichoeleza kuwa ni
kulinda heshima ya serikali.
Mbali na Prof. Muhongo, vigogo wengine waliong’oka kwa kashfa hiyo
ya uchotwaji wa Sh. 306 bilioni ni pamoja na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, Jaji Frederick
Werema na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna
Tibaijuka.
Chanzo ni Mwanahalisi,oline
No comments
Post a Comment