UKAWA WAMLIPUA WAZIRI MAGUFULI,WASEMA HAKUNA ALICHOKIFANYA SOMA HAPO KUJUA
Waziri wa Ujenzi Dr. John Magufuli akionnyesha michoro ya FLYOVER ambayo imekamilika kwaajili ya kufanyiwa kazi |
VYAMA vinavyounda
kundi la Umoja wa Katiba (Ukawa) vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi,
vimemshambulia Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magofuli kuwa, amekuwa akiainisha
miradi mingi ambayo utekelezaji wake haukamiliki kutokana na kupewa fedha ndogo
na Serikali. Anaandika Edson Kamukara … (endelea).
Akisoma maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani, Waziri Kivuli wa Ujenzi, Felix
Mkosamali aliainisha uamuzi wa Dk. Magufuli wa kununua kivuko cha Dar- Bagamoyo
kwa takribani Sh. 4 bilioni, kinachobeba abiria 300 na kinatumia saa tatu
kutoka Dar kwenda Bagamoyo, akisema ni upotevu wa fedha.
Mkosamali amesema inatia aibu kuona
baadhi ya wabunge wakijitutumia kumpongeza Magufuli kwa utendaji kazi mzuri kwa
kila wizara anayopita pasipo kuainisha udhaifu wa maamuzi yake ambayo
yameligharimu taifa.
“Ni jambo la ajabu kununua kivuko cha
kizamani au chakavu chenye spidi ndogo. Azam Bakhresa ana Meli inayotoka Dar
kwenda Zanzibar kwa muda wa dakika 90 tu na inabeba abiria 500 na kwa taarifa
tulizonazo, inauzwa kati ya Sh. bilioni 4 hadi 5.
“Kambi rasmi ya upinzni inaomba Bunge
lako kuunda Tume kuchunguza ununuzi wa kivuko hiki kibovu na cha kizamani,
kilichonunuliwa kwa bei kubwa huku kwa siku kikiweza kwenda Dar es Salaam na
kurudi Bagamoyo mara moja tu,”amesema.
Kwa mujibu wa Mkosamali, kivuko hicho
kimekosa abiria kwani wananchi wanaona bora kupanda daladala kuliko kivuko
kinachotumia saa tatu.
Hata katika mchango wake wa jumla kwa
bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2015/16, Mkosamali aligusia tena suala
la kivuko akisema, miradi hiyo inapelekwa katika baadhi ya maeneo ya viongozi
wakuu kwa upendeleo na kuacha mikoa mingine yenye mahitaji makubwa.
Madeni ya wakandarasi
Mkosamali amesema, katika mawasilisho ya
Magufuli aliliambia Bunge kwamba kulikuwa na kikosi kazi cha kuhakiki madeni
ambayo wizara mbalimbali zinadaiwa na wazabuni.
“Kambi upinzani inamtaka waziri
alieleze Bunge kwamba, kile kikosi kazi kilichoundwa na wizara ya fedha ili
kuhakiki uhalali wa madeni ya wizara yake, kimebaini inadaiwa kiasi gani na
wakandarasi pamoja na wazabuni wengine?
Amefafanua kuwa wizara hiyo, imekuwa
ikitengewa fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika bajeti kuliko wizara
zingine.
“Katika mwaka wa fedha wa 2014/2015,
wizara ya ujenzi imetengewa jumla ya Sh.bilioni 662.2 kwa ajili ya kutekeleza
miradi ya maendeleo. Hadi kufikia Januari, 2014 madeni ya makandarasi na
washauri yalikua ni Sh.bilioni 663.9.
“Wizara ya Ujenzi mpaka sasa inadaiwa
zaidi ya billion 800 na hakuna majibu juu ya ulipwaji wa madei hayo. Licha ya
uwasilishwaji wa bajeti ya wizara hii kuwa na kelele na mbwembwe nyingi ukweli
ni kwamba madeni ya wizara yanazidi fedha za maendeleo tunazaopitisha na Bunge
lako,”amesema.
Mkosamali ameongeza, “hata kwa mwaka
huu wa fedha, bajaeti ya maendeleo ni billion 890.6 kwa wizara na taasisi
zilizo chini ya wizara huku madeni yakiwa zaidi ya bilioni 800.Hivyo hakuna
uhalisia kati ya fedha za maendeleo zinazoombwa na madeni husika”.
Ameongeza kuwa, Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Wakandarasi (CRB) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Contractors
Association of Tanzania (CAT), Mhandisi Consolata Ngimbwa, alitoa kilio kwenye
mkutano wa mashauriano na maonyesho uliofanyika 14 Mei,2015 kwenye ukumbi wa
Mlimani City.
“Kwa uchungu mkubwa Mhandisi huyo
aliueleza umma kwamba wakandarasi watatu wamekufa kutokana na msongo wa kudaiwa
na watu waliokuwa wanatoa huduma katika kampuni zao, hii ni kutokana na
Serikali kutowalipa madeni yao pale wanapomaliza kazi,”amenukuu Mkosamali.
Kuhusu miradi ya barabara, Mkosamali
amesema, kila inapofika mwaka wa uchaguzi CCM imekuwa ikiahidi kujenga barabara
kwa lengo la kupata kura tu, lakini haitimizi ujenzi wa barabara walizoahidi.
Nao baadhi ya wabunge waliochangia,
Piter Msigwa, James Mbatia, John
Cheyo, Abass Mtemvu na wengine, walizungumzia kwa kirefu kuhusu msonagamano
jijini Dar es Salaam na kuitaka serikali ichukue hatua madhubuti za kumaliza
tatizo hilo.
Katika hitimisho la hoja yake, waziri
Magufuli alikiri hali ya msongamano kuwa tete na kuanisha mipango ya serikali
ya upanuzi wa barabara na ujenzi wa madaraja na barabara za juu lakini akaonya
kwamba wizara yake pekee haiwezi kumaliza tatizo hilo.
Pia kuhusu madeni ya wakandarasi,
Magufuli amewathibitishia wabunge kwamba wakandarasi wote na hasa wa ndani
watalipwa madeni yao yote kama ambavyo Rais Jakaya Kikwete ameahidi.
Chanzo ni Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni