HABARI KUBWA LEO,LOWASSA AJIPAKAA MASIZI,KEBEHI YAKE KWA KIKWETE KUMPONZA,SOMA HAPO KUJUA
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta, wakishuhudiwa na Steven Wassira pembeni |
SIKU moja baada ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, kuzungumza na waandishi wa habari na kumbeza Rais Jakaya Kikwete, kuhusu sera ya kilimo na makada wa CCM, Samuel Sitta na Dk. Harisson Mwakyemba, sasa kibao kimemgeukia, akidaiwa kutapatapa. Anaandika Edson Kamukara … (endelea).
Lowassa
ambaye alikuwa msaidizi wa Rais Kikwete kwa miaka miwili kama msimamizi wa
shughuli za Serikali kabla ya kujiuzulu kwa shinikizo la Bunge mwaka 2008 kwa
kashfa ya zabuni tata ya kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond
Development LLC, alisema serikali alikosea kuanza na kilimo kwanza na kuweka
elimu kando.
Pia, Lowassa alijitetea kuhusu
Richmond akisema hakula hata senti moja, isipokuwa aliyekuwa Spika wa Bunge la
Tisa, Samuel Sitta na Dk. Harrison Mwakyembe, aliyeongoza Kamati Teule,
walipika ripoti ya kashfa hiyo ili kumdhalilisha.
Kama ilivyobashiriwa kuwa, Lowassa
ameibua mzozo kwa kukinzana na utaratibu wa CCM unaowataka viongozi kupingana
au kukosoana kupitia vikao badala ya kufanya hivyo hadharani, baadhi ya makada
wamemjibu wakisema anatapatapa baada ya kuona hana nafasi ya kuteuliwa.
Licha ya Sitta na Mwakyembe
kutojitokeza kujibu chochote, lakini baadhi ya watu walio karibu nao, wamekidokeza
Chanzo changu kwamba, wamempuuza Lowassa kwa sababu ukweli wote kuhusu kashfa
ya Richmond uko wazi.
“Tumefuatilia kauli ya Lowassa kwa
waandishi wa habari, lakini tumeshauri viongozi hawa aliowakejeli wasijibu ili
kuvuruga mchakato wa uteuzi kwa sababu baadhi yao wataingia kwenye
kinyang’anyiro.
“Lakini kitendo cha kukebehi hata Rais
Kikwete ambaye alimwamini na kumpa madaraka makubwa ya uwaziri mkuu kuwa
serikali yake ilikosea kuanza na kilimo kwanza badala ya elimu, hii ni dalili
tosha kwamba Lowassa anatapatapa baada ya kubaini hana sifa za kuteuliwa
kugombea urais,” amesema mmoja wa makada aliyeomba kuhifadhiwa jina lake ili
kuepusha mtafaruku ndani ya chama.
Ameongeza kuwa, “anachokifanya sasa ni
visasi vya tukose wote. Huyu amekuwa serikalini na hayo anayozungumza ndizo
zilikuwa sera za CCM walizozinadi wakati wakisaka urais na badaye akapewa
uwaziri mkuu kusimamia hayo”.
Naye mbunge wa Nzega, Dk. Khamis
Kigwangalah (CCM), ambaye ametangaza nia ya kuomba uteuzi wa kugombea urais,
ameandika kupitia mtandao wa kijamii akisema, “kama Kamati ilimuonea Lowassa,
basi imuombe radhi na ituombe radhi Watanzania wote”.
Amekwenda mbali zaidi
akisema, “kama kweli Lowassa atagombea urais 2015, itakuwaje kwenye mijadala ya
uchaguzi na CCM itasimamaje kama itampitisha kuwa mgombea, kumuombea kura
wakati ilimuangusha bungeni kutoka
kwenye nafasi nyeti ya uwaziri mkuu?
Dk. Kigwangalah amehoji, CCM itatoa
majibu gani kuhusu kwa nini ilimuita Lowassa ‘gamba’ na ikatangaza hadharani
kuanza mchakato wa kuvua magamba ambao haukukamilika.
“Nilisema jana, Lowassa amefungua
pandora box, na kama atatangaza kweli kuwania urais, inabidi haya mambo yawekwe
wazi, yamalizwe, maana hauwezi jua ya kesho – ikitokea akawa mgombea wetu,
tutaanzia wapi kumnadi na kusema ni mtu safi, muadilifu, anayechukia rushwa na
ubadhirifu na kwamba anafaa kuwa Rais, wakati juzi tulisema hafai kuwa waziri
mkuu na tukamtoa?
“Nilisema kuwa, CCM haipaswi ku-risk
kuteua wagombea wenye mambo mengi ya kutolea maelezo kwa wananchi, ikifanya
hivyo itaangushwa asubuhi ya saa nne. Watanzania wa leo siyo wa juzi,”
ameandika Kigwangalah kupitia mtandao wa Jamii Forum.
Amefafanua kuwa Lowassa kama amekana
kuhusika na Richmond, sasa wanakamati inabidi wamjibu, waweke wazi, na wamjibu
kwa uwazi bila kuficha.
“Maana kama alionewa ijulikane na sisi
tuliohuzunishwa ama kufurahishwa na Bunge wakati ule tuujue ukweli. Yeye
anasema hakuhusika na ndiyo maana Kamati ya Mwakyembe haikuona haja ya kumwita
kumhoji. Ukweli tunauhitaji sana leo kuliko jana. Ukweli huu ni haki yetu,”
amesema.
Chanzo ni Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni