TANZANIA KUNAANDAA MICHUANO YA AFRIKA,SOMA HAPO KUJUA MICHUANO GANI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika
-CAF leo hii limeipa Tanzania uenyeji wa fainali za michuano ya Afrika ya
vijana umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.
Uenyeji huu ni hatua muhimu sana kwa Tanzania katika kukuza soka
la vijana na kwa hatua hii Tanzania itacheza moja kwa moja fainali hizi.
Katika kuandaa kikosi bora cha kushiriki fainali hizi Tanzania,
mwezi Juni mwaka huu TFF itaandaa mashindano ya Taifa ya vijana umri chini ya
miaka 13 na wachezaji bora wa mashindano haya wataunda kikosi cha mwanzo cha
Taifa kuelekea fainali za mwaka 2019.
TFF inamshukuru sana Rais Jakaya Kikwete na Mh. Fennela Mukangara
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kufanikisha maamuzi haya, na
inaamini ushirikiano huu wa Serikali na wadau wengine utafanikisha mashindano
haya mwaka 2019.
Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni