LOWASSA AWACHAFUA WAHARIRI WA HABARI NCHINI,WAZOMEWA KILA KONA SOMA HAPO KUJUA

By Malisa GJ,
Juzi Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kupitia umbrela
yao iitwayo "Jukwaa La Wahariri" walisafirishwa kwenda kuonana na
Eddo. Gharama za usafiri, chakula, malazi, communication allowance etc,
zililipwa na Eddo mwenyewe.
Jana wakafanya nae Press Conference, lakini yaliyotokea huko ni
aibu tupu. Nimeona baadhi ya maswali waliyouliza wahariri hao kwa Eddo
nikatokea kuwadharau sana.
Moja ya swali lililoulizwa na Hamis Dambaya ni hili,
"Mheshimiwa Kuna watu wanaandika juu ya afya yako kutetereka, lakini sisi
tunakuona fit ndio maana umetuita hapa.. je unalisemeaje hili?"
Hahahaa.! Nimecheka sana.. Hivi ni swali gani hili? Hili ni
swali la kuulizwa na mwandishi wa habari? Tena Hamis Dambaya aliyebobea katika
taaluma ya Habari kwa kiwango cha Masters katika Mass Communication?
Mwingine akauliza eti "kuna watu wanakuita Eddo badala ya
kukuita kwa hadhi yako Mhe.Edward Lowassa. Na wewe umekua ukiitika hata
unapoitwa Eddo, Je huoni hii ni kupunguza heshima yako ktk jamii?"
Hivi swali gani hili? Lowassa kuitwa Eddo au kuitwa Edward
kunahusiana vp na hatma ya nchi yetu ikiwa atakua Rais? Tulitegemea maswali
"critical" yenye kupima uwezo wa Lowassa kuongoza nchi hii sio kuhoji
eti anajisikiaje akiitwa "Eddo"..
Hii ni mifano tu lakini maswali yote yaliyoulizwa ni ya hovyo
hovyo na yanayoonesha wazi kuwa it was just "agenda setting".
Ni ugoigoi wa kiwango cha PhD kudhani Lowassa anapoteza heshima
yake akiitwa "Eddo" au Kikwete atapoteza heshima yake kwa kuitwa
"JK" au kudhani Nyerere alipoteza heshima yake kwa kuitwa "Mwalimu".
Ikiwa mnaona hivyo, basi kamwambieni mimi naendelea kumuita "Eddo".
Nimekerwa sana na aina ya maswali waliyoiluliza wahariri.
Ieleweke sipingi nia ya Eddo kugombea urais wa nchi hii. Eddo
kama mtanzania yeyote yule ana haki ya kugombea na kama watanzania watampa
ridhaa ana haki ya kutuongoza.
Nachopinga ni "ugoigoi uliotukuka" wa waandishi
wenzangu waliokubali kugeuzwa misukule ya wanasiasa na kufikia kugeuka mazuzu.
Waandishi wa aina hii hawafai kuendelea kuwepo kwenye "industry" ya
habari.
Wazungu husema "the one who decide what you eat can decide
what to speak". Yani anayeamua nini ule ndiye anayeamua nini uongee.
Nimeona yametimia kwa Jukwaa la wahariri.
Waswahili nao husema "anayemlipa mpiga zumari ndiye
anayechagua wimbo".. Eddo amewalipa wahariri na amewachagulia maswali ya
kumuuliza. This is shame.!
Najiuliza hivi kama Wahariri wamekubali kugeuzwa
"condom" na kutumika hovyo, vipi waandishi wa kawaida ambao wengi wao
ni maskini wa kutupwa?? Wale ambao ukiwaita kwenye event yako wanachukua hotuba
ya mgeni rasmi na kunyoosha mkono uwape chochote kisha wanaondoka kwenda kuwahi
event nyingine..
Yesu alipokua msalabani aliwauliza wale wayahudi "ikiwa
mmeutenda hivi mti mbichi, itakuaje kwa mti mkavu?"
Na mimi najiuliza ikiwa wahariri wamekubali kununuliwa kama
bidhaa, itakuaje kwa waandishi wa kawaida? Wahariri wengi wana nyumba,
mathalani makazi ya kueleweka. Wana magari, na mishahara yao si haba.
Lakini Waandishi wengi ni "pangu pakavu". Waajiri
wanawanyonya sana kwa kuwalipa mishahara kiduchu. Hawana makazi ya kueleweka..
Leo utamkuta Manzeshe kesho Yombo Buzza. Usafiri wao ni huu wa umma wa
"mama Uledi simama vizuri nipate pa kujishika". Sasa hawa kweli
watashindwa kununulika tena kwa bei chee?
Kuna wakati niliwahi kusema tasnia ya habari haiwezi kubadilika
kamwe kwa sababu sisi tunaotakiwa kuleta Mabadiliko hatujielewi.
Leo waandishi wanapiga kelele sana mishahara midogo lakini hawako tayari
kuungana kutetea maslahi yao. Uoga umewazidi, wanaishia kununuliwa.
Waandishi wengi wanaishi kwa kuunga unga kama treni ya tazara.
Mishahara yao ni aibu hata kutaja. Kuna baadhi yao hata mishahara hawapewi.
Wanaishi kwa "tip". Ukiandika story unasubiri story yako itoke. Ikiwa
Mhariri ataipitisha itoke utalipwa elfu 10 kwa story. Hivi huyu mwandishi
anaishije?
Halafu badala ya kuungana kupambania maslahi yao wanakubali
kunuliwa kama nyanya na vitunguu vya Ruaha Mbuyuni. This is shame.!
Nimelidharau sana Jukwaa la Wahariri. Hiki ndicho chombo
pekee kilichopaswa kuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya waandishi lakini
wamewageuka, wamewasaliti, wamewasahau wenzao.
Nashauri Jukwaa Hili livunjwe. Na ikiwa kweli Waandishi wako
"serious" na wanaumizwa na kukandamizwa na maslahi duni wanayopata,
nashauri waungane na kulikataa "Jukwaa feki, Jukwaa la Wachumia Tumbo,
Jukwaa la wapenda fursa, jukwaa la wahariri"
Malisa GJ || Your Partner In Critical Thinking.!
Hakuna maoni
Chapisha Maoni