SHIRIKA LA THE SAVE CHILDREN LAWAKUTANISHA WANASIASA NA WATOTO,WASEMA MENGI SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Meneja Mwandamizi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalohusika na Mambo ya watoto nchini la ‘The Save children’ bwana Mussa Mugita akizungumza na waandishi wa Habari |
WITO
umetolewa kwa Vyama vya Siasa nchini kuweka kipengele cha Watoto kwenye Ilani
zao za Uchaguzi unaotarajia kufanyika hapo baadae mwaka huu kwa kusema ndio
itakuwa njia ya kumkomboa Mtoto wa kitanzania anayetazamwa kama ametengwa na
Vyama hivyo vya Siasa nchini.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam
na Meneja Mwandamizi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalohusika na Mambo ya
watoto nchini la ‘The Save children’
bwana Mussa Mugita wakati wa Semina iliyowakutanisha Viongozi mbali mbali
wa Vyama vya siasa nchini pamoja na Baraza la Watoto lenye lengo la kujadili
changamoto mbali mbali zinazowakumba.
Ambapo Bwana
Mugita amesema kwa sasa mtoto wa kitanzania ni kama amesahulika na vyama vya
siasa katika ilani za uchaguzi jambo ambalo anadai kuwa limechangia kuteseka
kwa mtoto wa kitanzania na kumfanya akose mahitaji ya Muhimu.
Kwa mujibu
wa Meneja huyo amesema nia ya Shirika hilo ni kurudisha matumaini kwa mtoto wa
kitanzania ambaye amekuwa akitengwa na wanasiasa hayo kwa kuwakutanisha na
Viongozi mbali mbali wa Siasa wenye Jukumu la kutengeneza Ilani zao kwenye
Vyama vyao vya Kisiasa.
Kwa upande
wao Viongozi mbali mbali vya Vyama vya Siasa walihudhulia Semina hiyo walitoa
masikitiko yao kwa Serikali iliyopo Madarakani ambayo ni chama cha Mapinduzi
CCM kwa kuwatenga watoto kitanzania kwa kushindwa kuwapa Elimu bora pamoja na
Ulinzi jambo ambalo wanazidi dai limewakatisha tamaa watoto.
Wanasiasa huo ni Peter Mzirahi ambaye
ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini,Lilian Bendera ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Chama cha
NDC wate kwa pamoja waliitupia lawama Serikali nchini kwa kuwatenga watoto.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni