UAMSHO WAMPOPOA PINDA,WASEMA ASIJE KULAUMIWA MTU,SOMA HAPO KUJUA
Wafuasi kundi la Uamsho |
WIKI mbili baada ya Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda, kulieleza Bunge kuwa, hana taarifa za kunyanyaswa kwa viongozi wa
Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar, wanaokabiliwa na kesi ya
ugaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jumuiya sasa imeamua kumwandikia
barua kali.Aanaadika Pendo
Omary … (endelea).
Viongozi hao, wanadai kufanyiwa
udhalilishaji na mateso makubwa huko gerezani na hivyo kutishia kuanza mgomo wa
kula wakati wowote wakisema bora wapigwe risasi za
kichwa wafe kuliko kugeuza madai yao ya Zanzibar kuwa nchi inayojitegemea.
Kutoka na hatua
hiyo, wiki iliyopita katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri
Mkuu bungeni, baadhi ya wabunge wa Zanzibar, walimtaka Pinda aeleze ni kwanini
viongozi hao wanashtakiwa Bara wakati Zanzibar kuna mahakama.
Pia, walihoji ni
kwanini serikali isiunde tume ya kuchunguza madai hayo ya udhalilishaji kwa
masheikh hao ili kuondoa utata huo.
Hata hivyo, Pinda
katika jibu lake, alisema hakuwa na taarifa za uwepo wa unyanyasaji kwa
masheikh hao na hivyo kuomba apewe muda afuatilie ili kujua ukweli.
Kufuatia kauli hiyo ya Pinda, sasa Uamsho wamemwandia barua 23 Mei
mwaka huu, wakisema “Waziri Mkuu dai letu ni moja tu kusema kwamba bado
serikali ya CCM inamdanganya Rais Jakaya Kikwete, basi sisi Wanzanzibar dai
letu turejeshwe nchini kwetu Zanzibar.”
“Hatukatai
kushtakiwa, Zanzaibar tuna mahakama kuu kongwe kuliko ya bara. Tuna gereza kuu,
tuna serikali, tuna rais, tuna DPP tushtakiwe mahakama kuu ya Zanzibar sio
mahakama ya Kisutu wala mahakama ya Tanganyika iliyovaa koti la Muungano hatuna
imani nayo,” inasomeka sehemu ya barua.
Wanaongeza kuwa,
sheria ya ugaidi inatamka wazi kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya
Zanzibar ndizo mahakama pekee zenye mamlaka ya kisheria kusikiliza tuhuma za
ugaidi.
“Kwa kuwa kesi hiyo
ni ya kubuni kwa malengo machafu ya kisiasa ndio sababu ya kushtakiwa katika
mahakama ya Kisutu. Tumebambikiwa kesi ya ugaidi kutokana na msimamo wetu wa
wazi wa kudai mamlaka kamili ya nchi ya Zanzibar,”wanasema.
Barua hiyo,
inaongeza kuwa msimamo huo waliutangaza nchi nzima kupitia mikutano ya hadhara
kupitia taasisi za kiislamu Zanzibar na kuendeshwa na Jumuiya ya Taasisi ya
Uamusho na mihadhara ya Kiislaamu kwa kufuata taratibu zote na sheria za nchi.
“Kilichofuata ni
serikali ya CCM kuwashughulikia wale wote wanaonadi au vinara wa msimamo huo,
ushahidi wa hao ni kuwa hawakusalimika hata kidogo ndani ya chama,” insomeka.
Vile vile barua
hiyo, inawataja baadhi ya viongozi walioshughulikiwa na serikali ya CCM kwa
msimamo huo kuwa ni: Muasisi wa ASP na CCM aliyebeba kadi namba saba, Mzee
Hassan Nassor Moyo ambaye alifukuzwa.
Yupo pia Waziri Mkuu mstafu Jaji Joseph Warioba ambaye
alikashifiwa bungeni na vile vile aliyekuwa waziri na mtoto wa kiongozi wa
mapinduzi, Bargedia Yusuf Hamidi Mansour, aitwaye Yusuf Hamid.
Barua hiyo pia inamtaja aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud aliyefukuzwa kazi kwa kosa la kupiga kura ya
hapana kwenye Bunge la Katiba akipinga kuburuzwa na serikali ya CCM.
Kuhusu baadhi ya mateso ambayo viongozi hao wanayapata wakiwa
mahabusu, barua hiyo inasema ni kuhojiwa uchi wa mnyama, kulawitiwa na kuwekewa
vijiti sehemu za siri, kupigwa hadi kuzimia na kutoka taya, kulazwa na pingu
huku wakining’inizwa hadi asubuhi.
Wanadai mateso hayo yamewafanya kuendelea kupata maumivu, kutokwa
na haja kubwa bila kujua, kupoteza fahamu na kukojoa damu.
Barua hiyo ambayo
Chanzo changu imeoena nakala yake, Uamsho wanamwambia Pinda kuwa “tunapenda
serikali ya CCM ifahamu kuwa kutoa maoni huru ni haki yetu kikatiba na
hatutaacha kutumia haki wala hatutorudi nyuma”.
Chanzo ni Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni