HABARI KUBWA LEO.WASOMI WAMSHUSHUA LOWASSA,WASEMA NI MTU ANAYENUKA UFISADI NA HAFAI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Lowassa |
WACHAMBUZI wa masuala ya kisiasa, wamekosoa
mbwembwe zinazofanywa na baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
wanaotangaza nia ya kuomba uteuzi wa kugombea urais kupitia chama hicho,
wakisema sio kipimo cha ama wanafaa au la. Anaandika Yusuph Katimba …
(endelea).
Mhadiri Mwandamizi wa
Chuo cha Tumaini, Dk. Azavel Lwaitama, anasema pamoja na hekaheka kubwa za
wagombea lakini zipo njia za kuthibitisha kufaa au kutofaa kwake.
“Kwanza tujue anatoka chama gani? Chama
hicho kina sifa gani lakini pia je aliwahi kutetea maslahi ya umma alipokuwa
kwenye uongozi? Na wala si kupelekwa na upepo wa hekaheka zao,” anasema.
Dk. Lwaitama
anasema, kipindi hiki kila mgombea anataka kuwaonesha wananchi kwamba anafaa
lakini pia kwa wananchi wanapaswa kuonesha kuwa wamekomaa.
“Wagombea hawa
pamoja na kujitokeza kwa mbembwe lakini tuwapime. Je, ni wasafi kwa kiasi gani?
kwanini wanatumia nguvu kujitangaza? Malamiko ya wananchi katika chama hicho aliyateteaje?
amehoji.
Anasema, wapo
wanaojitokeza kutaka kugombea lakini hao hao chama wanachotaka kugombea tayari
kimewaita fisadi na chama hakijawasafisha na kimetembea nchi nzima kutaka avue
gamba, “na wakimpitisha mtu wa
namna hii mimi nitawashangaa sana.”
Dk. Lwaitama anasema,
wananchi wanapaswa kukumbuka ni kwa namna gani wanaojitokeza walipambana na
hoja zinazohusu matatizo yao katika jamii.
Anasema, wapo
waliokuwa na nafasi ya kukemea ufisadi ndani ya serikali lakini wakakaa kimya
na kwamba, watu wa namna hii kama walikuwa serikalini walishindwa, ni kipi
kinachoweza kuwafanywa wananchi wawaamini?
“Rushwa ndio
changamoto kubwa, sarafu inashuka, rasilimali zinaporwa, wananchi wanahangaikia
huduma za jamii na huyu anayekuja leo kutoka chama hicho alipaswa kuonesha
kuchukia kwa vitendo lakini walaa!.
“Hao hao
walipokuwa ndani walishindwa kukemea rushwa inayosababisha umasikini lakini
huku nje wanapiga kelele kwamba wanachukia rushwa,” amesema.
Ameongeza “Mtu wa namna hii hata akija na punda ili kudanganya
wananchi, hafai na wala hakuna kuangalia sura. Kama mtu hatukumwona akisimamia
ajenda za wananchi, huyo hafai kabisa,” anasema Dk. Lwaitama.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine-Mwanza (SAUT),
Dk. Francis Ng’atigwa, anasema, kitu kinachoweza kuwaweka wasaka madarasa hao
ni kubeba ajaenda za vyama vya na sio zao binafsi.
Anasema kuwa, sera ndio zinazoonesha vipaumbela kwa wagombea hao
na si kitu kingine. “Wananchi wanahitaji kusikia sera na sia ajenda binafsi za
wagombea. Naamini wagombea wanaobeba ajenda zao binasi watapotea kwa kukosa
‘support’ (kuungwa mkono),” amesema.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kiislam cha Morogoro, Bagesi Gaddafi,
anasema jambo la msingi kwa wanansiasa ni kujua matatizo ya wananchi na si
kutumia fedha, vitisho na ghiliba isipokuwa ni kuonesha uwezo halisi.
Anasema kuwa, haamini kama Watanzania bado wapo kwenye giza kwa
kufuata mkumbo ama mdundo wa sauti unakovuma pasipo sababu.
“Sidhani kama tupo kwenye zama hizo, zama za sasa ni zama za
kuchanganua mambo. Kwa bahati nzuri vyama vya upinzania vimekita mizizi kwa
kiwango cha kutosha,” anasema Gaddafi.
Mhadhiri huyo anasema kuwa, siasa za Tanzania kwa sasa zina sura
tofauti. ”Sura iliyopo ni ya kuhoji na kutaka majibu ya hapo kwa hapo.
“Unaweza kuona tu uchaguzi wa Serikali za Mitaa matokeo yake,
angalia watu wa vijijini wanavyokesha kusubiri kuandikwa katika daftari la
wapiga kura, hapa ndio unaweza kutathmini tuelekeako,” amesema.
Uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais umepangwa kufanyika
Oktoba 25 mwaka huu, na tayari makada wa vyamba mablimbali wanaendelea na
hekeheka za kutangaza nia pamoja na kuchukua fomu kuomba kuteuliwakuwa wagombea.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni