TUNDU LISSU ARUSHA KOMBORA SERIKALINI,SOMA HAPO KUJUA

TUNDU Lissu-Mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, amewasha
upya moto akisema, Rais Jakaya Kikwete ataondoka madarakani bila Katiba mpya
aliyowaahidi Watanzania takriban miaka mitano iliyopita. Anaandika Edson Kamukara … (endelea).
Lissu ambaye pia ni mbunge wa Mbunge wa
Singida Mashariki (Chadema) na msemaji mkuu wa upinzani kwa Wizara ya Katiba na
Sheria, ametoa kauli hiyo ikiwa ni wiki moja tangu alipoibua mjadala bungeni
akisema Serikali ya CCM ni chovu inapaswa kuondolewa madarakani.
Akisoma maoni ya kambi hiyo kwa
makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa
fedha 2015/16, Lissu amesema “31 Disemba, 2010, Rais Kikwete alilihutubia Taifa
na kuwaahidi Watanzania kwamba itakapofika 26 Aprili, 2014 – wakati waGolden Jubilee ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – nchi yetu itapata Katiba Mpya.”
L issu amesema Golden Jubilee ya
Muungano wetu, yaani 26 Aprili, 2014, ilipita bila ya nchi kuwa na Katiba mpya
iliyoahidiwa na Rais Kikwete.
“Baadaye tarehe 2 Oktoba ya
mwaka huo, ‘Bunge Maalum’ lenye wajumbe wa chama cha waliohusika na EPA, Richmond/Dowans, Tegeta Escrow, Operesheni
Tokomeza wafugaji na Operesheni kimbunga dhidi ya Watanzania waishio mipakani,
lilipitisha Katiba Inayopendekezwa.
“Hiyo ni baada ya kura
iliyopigwa na wafu waliokuwa wametangulia mbele ya haki, mahujaji waliokuwa
wanampiga shetani mawe katika Mlima Ararat, Makka nchini Saudi Arabia, wagonjwa
waliokuwa wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini India na wajumbe wengine
wasiojulikana kwa majina wala walikokuwa wakati wa kura hiyo,”amesema.
Ameongeza kuwa, baada ya
kukabidhiwa Katiba Inayopendekezwa katika sherehe iliyofanyika hapa Dodoma,
Rais Kikwete aliwaahidi Watanzania – kwa mara nyingine tena – kwamba itapigiwa
kura ya maoni mnamo 30 Aprili, 2015.
“Ahadi hiyo ilirudiwa rudiwa
na kila kiongozi wa CCM na Serikali yake ndani na nje ya Bunge hili tukufu.
Hata hivyo, tarehe 30 Aprili ilipita na kura ya maoni iliyoahidiwa na Rais
Kikwete haikufanyika.
“Leo ni wiki ya tatu tangu
tarehe ya kura ya maoni ipite bila kura hiyo kufanyika na watu wale wale wa
chama kile kile kwa maneno yale yale wanatuahidi kwamba kura ya maoni
itafanyika katika tarehe ambayo hawaitaji,” amesema.
Lissu ameongeza kuwa, “Wahenga
wetu walisema ‘wajinga ndio waliwao.’ Kwa sababu hiyo, Mtanzania yeyote
atakayeamini ahadi hewa za watu hawa na chama chao asije akashangaa wala
kulalamika atakapoliwa tena.”
Amesisitiza kuwa, “kwa kifupi,
hakuna uhakika wowote kwamba kutakuwa na kura ya maoni ili kuhalalisha Katiba
Inayopendekezwa na CCM. Badala yake, uhakika pekee tulio nao ni kuwa Rais
Kikwete ataondoka madarakani bila Katiba mpya aliyowaahidi Watanzania.”
Kuhusu fedha za Mahakama na
uhuru wa mahakama, Lissu alirejea maoni ya kambi hiyo kwa mwaka wa fedha
2011/12, kuwa“tatizo kubwa linalozikabili mahakama zetu sio uhaba wa uwezo wa
kusimamia fedha zinazotolewa kwa ajili yao, bali ni uhaba wa fedha zenyewe.”
Amesema, katika miaka mitano
ya maisha ya Bunge, Serikali hii ya CCM haijawahi kuipatia Mahakama ya Tanzania
fedha za kukidhi mahitaji yake kwa mujibu wa vipaumbele vyake.
“Ukweli ni kwamba serikali hii
ya CCM haijawahi kukana jambo hili. Wimbo wake ni ule ule wa miaka yote wa
ufinyu wa bajeti,” amsema.
Lissu amesema, hali ya
miundombinu ya mahakama imekuwa mbaya na ya kusikitisha katika miaka hii mitano
ya maisha ya Bunge.
Kuhusu haki za binadamu,
amesema kuna kila dalili za kuonyesha kwamba waliyoyapigia kelele badala ya
kupungua, yameongezeka. Kwamba, hali ya haki za binadamu katika miaka mitano ya
maisha ya Bunge inatisha na imezidi kuwa mbaya.
“Mauaji na mashambulio dhidi
ya viongozi wa kidini na waumini wao na sehemu zao za ibada yaliyotokea kati ya
mwaka 2012 na 2013 hayajatatuliwa hadi leo. Hakuna mtu yeyote ambaye
ameadhibiwa kwa mauaji ya padre mmoja wa Kanisa Katoliki Zanzibar.
“Hakuna aliyeadhibiwa kwa
shambulio la risasi na la tindikali dhidi ya mapadre wengine wawili wa kanisa
hilo huko huko Zanzibar wala kwa shambulio la tindikali dhidi ya msaidizi wa
Mufti wa Zanzibar,”amesema.
Pia ameongeza kuwa,hakuna
aliyetiwa hatiani wala kuadhibiwa kwa kuhusika na shambulio la bomu katika
Kanisa Katoliki Olasiti- Arusha, lililoua watu watatu na kujeruhi wengine
wengi.
“Serikali ya CCM haijatoa
taarifa yoyote rasmi hadharani au bungeni juu ya wahusika wa mauaji na
mashambulio hayo na sababu zake. Mauaji na mashambulio ya waandishi wa habari
na wanaharakati wengine kama madaktari yaliyotokea kati ya 2012 na 2013
hayajatatuliwa pia.
“Maafisa wa Jeshi la Polisi
walioamuru mauaji ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi hawajachukuliwa hatua
yoyote. Badala yake, aliyekuwa kamanda wa polisi hao amepandishwa vyeo na
kuhamishiwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,”amesema Lissu.
chanzo ni Mwanahalisi oline
Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni