NEC KUWEKA MAMBO HADHARANI YA MAJIMBO YA UCHAGUZI NI JUNI 30,SOMA HAPO KUJUA
pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa NEC, Kailima Ramadhani Picha na michuzi.blog |
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema kuwa,
kati ya tarehe 13 Mei hadi 31 mwaka huu, ndio muda uliotengwa kwa ajili ya
kupokea mapendekezo ya ugawaji wa majimbo. Anaandika Sarafina Lidwino…(endelea).
Kaimu Mkurugenzi wa NEC, Kailima
Ramadhani, amewaeleza waandishi wa habari leo kwamba, takwimu za idadi ya watu
zitakazotumika ni za makisio mpaka mwaka 2015 na zitapatikana Ofisi ya Takwimu
ya Taifa.
Amesema kwa mujibu
wa takwimu “Population quota”, kwa upande wa majimbo ya mijini itakuwa 325,000
na kwa majimbo ya vijijini ni 235
,000, hivyo kuyataka majimbo ambayo
hayajatimiza idadi hiyo ya watu wasilete maombi isipokuwa tu kama ni
halmashauri mpya.
Ramadhani amefafanua
kuwa, vigezo vitakavyotumika katika ugawaji huo ni idadi ya watu, ambapo
watazingatia ongezeko la watu hadi kufikia Julai mwaka huu, upatikanaji
wa mawasiliano, ambapo watazingatia uwepo wa miundombinu kama barabara.
Vigezo vingine ni
hali ya kijiografia, ambapo litaangaliwa jimbo lipo sehemu gani kama ni mlimani
au bondeni, mazingira ya muungano, uwezo wa ukumbi wa Bunge na viti
maalumu vya wanawake ambapo watatenga kiasi cha zaidi ya asilimia 30 kwa ajili
ya wabunge wanawake.
Amesema, watazingatia
hali ya kiuchumi kwa kushirikisha Tamisemi, ukubwa wa eneo, mipaka ya
kiutawala, jimbo moja lisiwe ndani ya wilaya au halmashauri mbili, kata
moja isiwe ndani ya majimbo mawili na mpangilio wa maeneo ya makazi ya watu
yalipo.
Kwa mujibu wa Ramadhani, utaratibu utakaotumika kuwasilisha maombi
hayo ni wananchi kuwasilisha maoni yao kwa Mkurugenzi wa
halmashauri husika, kisha halmashauri itayawasilisha kwa Katibu Tawala wa
Mkoa (RAS).
Amesema baada ya hapo RAS atawasilisha maombi katika kikao cha
kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) ili kupata maoni zaidi. Kwamba, baada ya hapo
yataletwa NEC na kuanza kufanyiwa kazi.
Chanzo ni Gazeti la mwanahalisi oline
No comments
Post a Comment