HABARI KUBWA LEO-SAMWEL SITTA KUMWAGA MANYANGA YA RICHMOUND,KUSEMA KILA KITU,ASEMA LIWALO NA LIWE,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Samwel Sitta |
WAZIRI wa
Uchukuzi,Samwel Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge llilopita anatalajia kuweka
mbivu na mbichi ambazo zilizofichiki kwenye Kampuni Tata ya Richmound,mtandao huu
umedokezwa,Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Kwa Mujibu wa Vyanzo vyetu zinasema kwa
sasa Waziri huyo Mwandamizi anatalajia
kuzungumza na kundi la watu linalojiita
“Jukwaa la Wahariri” kuweka
bayana ukweli wote ambao unadaiwa kutowekwa hapo awali.
Kuibuka kwa Waziri Sitta pamoja na
Mwakyembe kuna kuja ikiwa imepita wiki moja baada ya Aliyekuwa Waziri Mkuu
Edward lowassa kuvunja ukimya na kusema kamati ya Bunge iliyoundwa Bunge la Samwel Sitta ambayo iliongozwa na Dk
Mwakyembe ilimuonea kwenye sakata hilo.
Lowassa ambaye ni miongoni mwa Makada
ndani ya CCM ambao wanautaka urais wa udi na uvumba kwenye chama hicho,awali
alikuwa Waziri Mkuu wa mwazo kwenye Utawala wa Rais Kikwete na alijiuzulu kutoka na
kutuhumiwa na Kamati iliyoundwa na kuchunguza kampuni ya Richmound ambapo kamati
hiyo ilimtuhumu Lowassa kutumia ubabe wake kuipa zabuni kampuni hiyo kinyume na
taratibu huku ikiwa haina uwezo wala pesa.
Chanzo hicho kimeudokeza mtandao huu nakusema Dk Mwakyembe na Samwel Sitta wataweka bayana suala hilo kunatokana
na kuchukizwa na kauli aliyoisema Lowassa ambaye ni Mbunge wa Munduli CCM .
“Kusema ukweli Serikali ya CCM
imechukizwa sana na kauli ya Lowassa kuzungumzia sakata hili ambazo limekiponza
chama sana mpaka kukosa kura nyingi kwenye uchaguzi wa mwaka 2010,leo
amelirudisha tena,na ndio maana Sitta na mwakyembe wameamua kuliweka bayana
bora wafanye hivyo”
“Nakwambia
utasikia mengi sana kwenye mkutano na Wahariri ambao unatarajia kufanyika mda
wowote kuanza sasa,na utaona mengi sana mwaka huu,”
Maoni 3
Yaani walificha ukweli kwa makusudi? Ndicho wanachokiri, na Mwakyembe amesema hawakusema kila kitu eti ili kulinda heshima ya Lowassa. Yaani hao jamaa wanaona ni muhimu zaidi kuangalia maslahi ya mtuhumiwa wa ufisadi kuliko maslahi ya Taifa. Huu utamaduni wa kulindana ambao umejengeka katika CCM ni sherti ukomeshwe ifikapo Oktoba mwaka huu.
Na sita ukimaliza utuambie ufisadi wako wa kujenga ofisi ya bunge urambo kama vile utakuwa spika maisha yoote
Nachotaka kujua siku zotee walikuwa wapii kusema aliyopitia lowasa mpk baada ya miaka saba na watueleze Jk anahusika vipi na Richmond maana lzm km Rais ajue kabla sasa toeni ufafanuzi vzr
Chapisha Maoni