MAKADA WA CCM WAGOMBANIA IKULU,WASIRA,MWIGULU NAO WAJITOSA,VIJEMBE VYATAWALA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Steven Wassira ambaye leo ametanga Rasm kuwania Urais ndani ya CCM |
WIMBI la
Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM,kugombania nafasi ya kumrithi Rais anayemaliza Mda wake Jakaya
kikwete hapo baadaye mwaka huu, limezidi kuongezeka huku Makada hao wakiweka Vijembe na majungu vikitawala. Anaandika
KAROLI VINSENT Endelea nayo.
Mlango huo ulifunguliwa jana na Waziri Mkuu
aliyejiuzulu kwenye Kashfa ya Ufisadi kwenye Kampuni Tata ya Richmound Edward
Lowassa nyumbani kwake Arusha na kutangaza Safari ya matumaini ambayo yenye
Ajenda ya kutaka Urais.
Hatimaye leo wameibuka Makada wengine
wa Chama hicho kikongwe barani Afrika kilichopo madarakani na kutangaza kutaka
Urais huko wakiweka Sera ambazo wanadai zitamsaidia mtanzania.
Makada
hao ni Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba ambaye naye amejitokeza na kutaka Urais
huku akiweka Vipaumbele mbali mbali pindi atakapopitishwa na CCM.
Akitangaza azma hiyo Kwenye Chuo kikuu
cha Mipango mkoani Dodoma huku akishuhudiwa na mamia ya Watanzania amesema nia
ya Sababu iliyomsukuma kuitaka nafasi hiyo kubwa inatokana na kushuhudia
watanzania wakiteseka na Umasikini huku wakiwa na Rasilimali lukuki.
“Mimi
mwenyewe umasikini naujua maana nilipomaliza shahada yangu ya pili pale Chuo
kikuu nilikuwa masikini sina kazi,harafu nilikuwa nimeoa nikaamuna kujiingiza
hata kwenye kazi za kubeba zege ,ndio maana naitaji nafasi ya Urais kwa lengo
la kuwasaidia watanzania ambao wamekumba na umasikini lukuki”
Pamoja na hayo Mwigulu akusita kuzungumzia
suala la kilimo ambapo amesema akipata nafasi hiyo atatumia kila njia kuweka kuongeza
viwanda ndani ya nchi ili kuweza kumuokoa mkulima pindi atakapouza mazao yake.
Sanjari na Mwigulu Nchemba kuibuka kutaka
Urais, hapo mwanzo pia mwengine ni Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Steven
Wasira ambapo nae ametangaza Rasmi kuitaka nafasi ya Urais na kusema pindi
akipewa nafasi atainua sekta ya Kilimo ambayo anadai ni uti wa mgongo.
VIJEMBE VYA TAWALA.
Licha ya
Makada hao watatu kutangaza nafasi hiyo Vijembe vilitawala vya kupondana wao
kwa wao.
Lowassa
Wa kwanza
kurisha Vijembe alikuwa ni Waziri Mkuu Aliyejiuzulu Edward lowassa ambaye
amesema anashangaa watu wanaoutaka Urais huku hata awajakaa madarakani kwa mda
mrefu.
“Mimi
nimpigana kwenye Vita vya Iddi Amin najua changamoto zake tena ni nauzoefu hebu
waulizeni hao wengine wanamiaka michache harafu anautaka Urais”amesema Lowassa
Mwigulu ajibu kijembe hicho
“unaweza kukaa madarakani kwa mda mrefu watu
wanaangalia umefanya nini?kwasababu unaweza kukaa mda mrefu Serikalini huku
ukaitia Serikali hasara ya Mabilioni ya pesa”amesema Mwigulu
Hakuna maoni
Chapisha Maoni