Zinazobamba

HABARI KUBWA LEO-SAMWEL SITTA KUMWAGA MANYANGA YA RICHMOUND,KUSEMA KILA KITU,ASEMA LIWALO NA LIWE,SOMA HAPO KUJUA


Pichani ni Samwel Sitta
WAZIRI wa Uchukuzi,Samwel Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge llilopita anatalajia kuweka mbivu na mbichi ambazo zilizofichiki kwenye Kampuni  Tata ya Richmound,mtandao huu umedokezwa,Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
       Kwa Mujibu wa Vyanzo vyetu zinasema kwa sasa Waziri huyo Mwandamizi  anatalajia kuzungumza na kundi la watu linalojiita  “Jukwaa la Wahariri”  kuweka bayana ukweli wote ambao unadaiwa kutowekwa hapo awali.
      Kuibuka kwa Waziri Sitta pamoja na Mwakyembe kuna kuja ikiwa imepita wiki moja baada ya Aliyekuwa Waziri Mkuu Edward lowassa kuvunja ukimya na kusema  kamati ya Bunge iliyoundwa  Bunge la Samwel Sitta ambayo iliongozwa na Dk Mwakyembe ilimuonea kwenye sakata hilo.
     Lowassa ambaye ni miongoni mwa Makada ndani ya CCM ambao wanautaka urais wa udi na uvumba kwenye chama hicho,awali alikuwa Waziri Mkuu wa mwazo kwenye  Utawala wa Rais Kikwete na alijiuzulu kutoka na kutuhumiwa na Kamati iliyoundwa na kuchunguza kampuni ya Richmound ambapo kamati hiyo ilimtuhumu Lowassa kutumia ubabe wake kuipa zabuni kampuni hiyo kinyume na taratibu huku ikiwa haina uwezo wala pesa.
      Chanzo hicho kimeudokeza mtandao huu nakusema Dk Mwakyembe na Samwel Sitta  wataweka bayana suala hilo kunatokana na kuchukizwa na kauli aliyoisema Lowassa ambaye ni Mbunge wa Munduli CCM .
       “Kusema ukweli Serikali ya CCM imechukizwa sana na kauli ya Lowassa kuzungumzia sakata hili ambazo limekiponza chama sana mpaka kukosa kura nyingi kwenye uchaguzi wa mwaka 2010,leo amelirudisha tena,na ndio maana Sitta na mwakyembe wameamua kuliweka bayana bora wafanye hivyo”
“Nakwambia utasikia mengi sana kwenye mkutano na Wahariri ambao unatarajia kufanyika mda wowote kuanza sasa,na utaona mengi sana mwaka huu,”


Maoni 3

Mbele alisema ...

Yaani walificha ukweli kwa makusudi? Ndicho wanachokiri, na Mwakyembe amesema hawakusema kila kitu eti ili kulinda heshima ya Lowassa. Yaani hao jamaa wanaona ni muhimu zaidi kuangalia maslahi ya mtuhumiwa wa ufisadi kuliko maslahi ya Taifa. Huu utamaduni wa kulindana ambao umejengeka katika CCM ni sherti ukomeshwe ifikapo Oktoba mwaka huu.

zilageze@yahoo.com alisema ...

Na sita ukimaliza utuambie ufisadi wako wa kujenga ofisi ya bunge urambo kama vile utakuwa spika maisha yoote

zilageze@yahoo.com alisema ...

Nachotaka kujua siku zotee walikuwa wapii kusema aliyopitia lowasa mpk baada ya miaka saba na watueleze Jk anahusika vipi na Richmond maana lzm km Rais ajue kabla sasa toeni ufafanuzi vzr