HABARI KUBWA LEO-HATIMAYE KIKWETE ASAINI SHERIA YA MITANDAONI,WADAU WA HABARI WALIA NAYE,WAZIRI MBARAWA ASEMA HAKUNA JINSI,SOMA HAPA KUJUA
![]() |
pichani ni Rais Jakaya Kikwete |
LICHA ya
wadau mbali mbali wakiwemo wadau wa Mambo ya Habari,wanasiasa pamoja na
wanaharakati kumtaka Rais Jakaya Kikwete asiusaini Mswaada wa Uharifu wa Mitandao
nchini wa Mwaka 2015-
Hatimaye ni kama Rais Kikwete amepuuza
kilio hicho na kusiani Mswaada huo na
kuwa Sheria Rasmi na kuanzia kutumika kuanzia kesho.Anaandika KAROLI VINSENT
endelea nayo.
Akithibitisha kusainiwa kwa Mswaada huo
na kuwa sheria Rasmi na Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa leo tarehe 8 mwezi wa tano mwaka huu,jijini Dar es Salaam, Wakati wa Mkutano na
Waandishi wa Habari ambapo amesema Baada ya Mswaada huo kupitia sehemu mbali
mbalina kuonekana hauna Tatizo lolote ndio ukamfanya Rais Kikwete kusiani
Mswaada huo.
Waziri Mbarawa amesema Sheria hiyo
itasaidia kupunguza Makosa mbali mbali ya watu wanaofanya kwa Makusudi kwenye Mtandao Jambo ambalo anadai italiweka
Taifa salama na kuondokana na Tabia iliyojijengeka kwa Baadhi ya watu kuandika
Habari na kusambaza Taarifa za upotoshaji kwenye Mitandao ya Kijamii.
Pamoja na hayo Waziri Mbarawa amesema kwa
sasa baada ya Rais Kikwete kusaini hatua inayofuata ni kazi ya Wizara hiyo
kuwaelimishwa wananchi kuijua sheria hiyo ili
kuanza kutimika Rasmi.
![]() |
Pichani ni waziri wa Mawasiliano,Sayansi na TeknolojiaProfesa Makame Mbarawa picha na Maktaba |
Aidha,Waziri huyo amesema kwa wale
wadau mbali mbali wa Masuala ya Habari na wanasiasa pamoja na Wanaharakati
ambao walikuwa wanaubeza Mswaada huo,wanatakiwa kuwasilisha hoja zao kwenye
Wizara yake ili hatua zichukuliwe kwenye Vipengele ambavyo Wizara hiyo itaviona
labda vitakuwa na Utata .
Vilevile akawataka Watanzania kuipokea
sheria hiyo kwa Manufaa makubwa kutokana na Uharifu wa Mitandao hivi sasa ambao ulikuwa unawasumbua.
Kusaniniwa kwa Msaada kunatafsiliwa na
wadau mbali mbali wa Masuala ya Habari nchini ni kama umeendelea kunyonga Uhuru
wa Habari nchini kutokana na Sheria hiyo kuwepo na Vifungu Kandamizi kwa watu
wanaotoa Taarifa kwa Umma kwa njia ya Mitandao.
Wadau mbali mbali wa masuala ya Habari
waliokutana tarehe 2 ya mwezi huu Mkoani Morogoro siku ya Vyombo Vya Habari
Duniani walimtaka Rais Kikwete kutosaini Mswaada huo kwani utaiweka Njia panda
Taifa na wakadai Uhuru wa Habari unazidi
wambwa Msalabani kutokana na Vipengele vilivyopo kwenye Sheria hiyo mpya.
Wanasheria wananena
Wanasheria
Mmoja Maarufu hapa Jijini aliyezungumza na Mtandao huu amesema kitendo cha Rais
kikwete kusaini Mswaada huo na kuwa sheria ni kama kuua Rasmi Uhuru wa kutoa
habari na kupata Habari.
“kusema
kweli Rais Kikwete amenisikitisha sana kusaini Mswaada wenye utata leo Rais
Kikwete wakati anaingia madarakani alitoa uhuru mkubwa wa kujieleza na kutoa
maoni inakuwaje sasa anakubali kusaini mswaada wenye utata kama huu ambao
unamkosa chungu mzima”amesema Mwanasheria.
Gwaji huyo wa Sheria alizidi kuongea
kwa Uchungu amesema kwa sasa Jinsi hali anavyoiona basi watanzania wengi
wajiadhali kuishia magerezani kutokana na kuwa na Vipengele anavyodai vina
utata.
No comments
Post a Comment