WAZIRI WA KIKWETE AWAKIMBIA WANAHABARI,SOMA HAPA KUJUA

FENELLA Mukangara-Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ametia doa hafla ya utoaji tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania
(EJAT) 2014, zinazoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT). Amealikwa hakuja
wala hakutuma mwakilishi. Anaandika Mwandishi
Wetu… (endelea)
Tuzo hizo zimekabidhiwa jana na Makamu wa
Rais, Dk. Mohammed Gharib Billal ambapo waandishi 44 walioteuliwa na majaji
walichuana katika makundi 21.
Siri
ya “utoro” wa Dk. Mukangara ilifichuka wakati Jaji mkuu wa jopo lililopitia
kazi za waandishi hao, Chrysostom
Rweyemamu alipokuwa akitoa taarifa ya mchakato mzima ulivyokwenda mbele ya
mgeni rasmi.
Rweyemamu alianza kwa kuwatambua wageni
waalikwa kulingana na nafasi zao za uongozi. Alimtaja Dk. Mukangara lakini
alipoinua macho meza kuu, akasita kidogo na kusema “simuoni waziri
Mukangara…nadhani hajafika.”
Kwa mujibu wa ratiba, Dk. Mukangara ndiye
alipaswa kusema neno fupi la kumkaribisha mgeni rasmi ahutubie hadhara, badala
yake kazi hiyo ikabidi ifanywe na Jaji mstaafu Thomas Mihayo-aliyepia Rais wa
MCT.
Haikufahamika
mara moja sababu ya kutofika kwake au mwakilishi wake, lakini pia MCT hawakutoa
ufafanuzi wowote kama alikuwa ameomba udhuru au la.
Hali
hiyo iliibua minong’ono ya hapa na pale ukumbini. Baadhi ya waandishi wakadai
kwamba amekwepa asibanwe kuhusu Muswada wa Habari (2015), uliosomwa na Serikali
kwa mara ya kwanza bungeni ukiwa umeacha maoni ya wadau.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi tuzo kwa washindi, Dk. Bilal aliwata waandishi kufanya kazi
kwa kuzingatia maadili na weledi hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu ili
kuisaidi jamii kuepuka vurugu.
Washindi bora wa jumla kwa mwaka 2015 ni
Mkinga Mkinga na Lucas Liganga wa gazeti la The Citizen huku tuzo ya
mwanahabari bora wa maisha ikitwaliwa na Jenerali Twaha Ulimwengu.
Washindi hao pamoja wengine walikabidhiwa
zawadi mbalimbali zikiwemo tuzo, fedha, runinga, kompyuta mpakato, simu na
vyeti vya utambuzi.
Chanzo ni
Gazeti la Mwanahalisi.oline
No comments
Post a Comment