MGOMO WA MADEREVA TENA JUMATANO,WASEMA WAMECHOKA NA UGEUGEU WA WAZIRI KABAKA,SOMA HAPA KUJUA
![]() |
Katibu Mkuu wa Chama cha Madareva Tanzania (TTDA), Rashid Sahel akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu adhima yao ya kukutana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda |
UMOJA wa Madereva Tanzania
(TTDA), wamepanga kumwandikia barua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuomba akutane
nao kusikiliza kilio chao, baada ya Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka
kupuuza matakwa yao. Anaandika Sarafina Lidwino…(endelea).
Katibu
Mkuu wa TTDA, Rashid Salehe amesema “tulitaka kuwa na mkutano siku ya kesho,
lakini kutokana na siku hiyo kuingiliana na siku kuu ya kitaifa, hatutanya.
Badala yake tutafanya Aprili 29 mwaka huu, maeneo ya Kimara Resourt.”
Kwamba, hayo sio maandamano, bali kikao
cha kawaida, hivyo jeshi la polisi wasiwawekee hofu. Anaongeza kuwa “usafiri
hautakuwepo siku hiyo…tutalaza vyombo”.
Hatua hiyo, imekuja baada ya mgomo wa
madereva uliotokea 11 Aprili mwaka huu, wakipinga kanuni mpya zilizopitishwa na
Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani za kuwataka kwenda kusoma wakati
wa kuhuisha leseni zao.
Kufuatia mgomo huo ulioleta madhara
makubwa kwa abiria na uchumi wa nchi, waziri Kabaka aliwaahidi madereva
hao kuwa, suala la kurudi darasani kipengere hicho atakiondoa na kurejesha
utaratibu wa zamani na kwamba hawatalipa ada ya Sh.580,000 kama ilivyokuwa
imeainishwa.
Pia aliwaambia kuwa, wizara imeanzisha
mfuko wa watumishi wanaoumia kazini ambao ni lazima waajiri wao wawalipie ili wafanyakazi
wote wanufaike na mfuko huo.
Baada ya makubaliano hayo,
Kabaka aliomba kukutana na uongozi wa madereva hao 18 Aprili, ili kujadili
suala hilo na wajue jinsi ya kutatua matakwa yao.
Salehe amewaeleza waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam kuwa, “hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na waziri huyo,
hivyo ameendelea kuyapuuza matakwa yetu.”
Amesema, kutokana na hilo,
walipanga kuwa na mkutano utakao wajumuisha madereva wote nchini ili kujadili
suala hilo.
Kwa mujibu wa Salehe, lengo la
mkutano huu ni kuwajuza wenzao kilichojili siku walipokutana na waziri Kabaka
ili kuona hatua gani za kuchukua wakati wakisubiri jibu la serikali.
Chanzo ni
Gazeti la Mwanahalisi.oline
No comments
Post a Comment