HABARI KUBWA LEO-MBUNGE LEMA AMLIPUA RAIS KIKWETE,AFICHUA SIRI NZITO SOMA HAPA KUJUA

GODBLESS Lema-Mbunge wa Arusha Mjini
(Chadema), amewasihi wananchi kuipigia kura ya ‘hapana’ Katiba inayopendekezwa,
akidai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinataka kutumia udhaifu wa katiba hiyo
kumbakiza Rais Jakaya Kikwete, madarakani hadi 2019. Anaandika Mwandishi wetu, Shinyanga … (endelea).
Akihutubia mamia ya wafuasi wa
Chadema mjini Shinyanga katika viwanja ya Mahakama ya Mwanzo, Lema ambaye pia
ni Waziri Kivuli kwa Wizara ya Mambo ya Ndani, amewataka wananchi kujiandikisha
kwa wingi katika daftari jipya la kudumu la wapiga kura ili kuikataa katiba
hiyo mpya isipite.
Huku akishangiliwa
na wananchi, mbunge huyo alinukuu kifungu cha katiba hiyo inayopendekezwa,
akisema kuwa endapo itapita, Rais Kikwete na timu yake yote wataendelea kubaki
madarakani mpaka pale kipindi cha mpito cha miaka minne kitakapokamilika.
Lema aamesema
“uhalali wa viongozi wa Jamhuri ya Muungano waliopo madarakani hivi sasa
umeelezwa wazi ndani ya katiba inayopendekezwa kwenye ibara za 285, 286 na 288.
Wananchi isomeni katiba mvielewe vifungu hivyo.”
Amesema hivi sasa
viongozi wa CCM wanahangaika na kuwashinikiza watanzania kuipigia kura ya
“ndiyo” katiba ili ipite na waweze kuendelea na nyadhifa zao. Kwamba, “dawa
pekee ya kunusuru hali hiyo ni kupiga kwa wingi kura za “hapana.”
Lema alinukuu
ibara ya 285 ya katiba inayopendekezwa katika sehemu ya tatu ambayo
inayozungumzia utumishi wa umma kuhusu kuendelea kuwepo kwa Rais kwamba
ataendelea kushika madaraka hayo hadi kipindi cha mpito kimalizike.
Ameongeza kuwa, ibara ya 288 katika kifungu kidogo cha (1) inaendelea
kuwataja viongozi wengine watakaoendelea na nyadhifa zao mpaka pale katiba
inayopendekezwa itakapoanza kutumika rasmi.
“Viongozi haoni
Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, mawaziri, naibu mawaziri, wabunge, majaji na
watumishi wote wa umma katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wataokuwa
madarakani kabla ya kutumika kwa katiba hiyo, nyadhifa zao zitaendelea
kutambulika,”amesema.
Amefafanua kuwa
CCM imeweka mtego ambao watanzania wengi hawajaubaini ili washawishike kuipigia
kura ya “ndiyo” katiba hiyo na ikipita ndipo waelimishwe kwamba viongozi wote
walioko madarakani watawajibika kuendelea na nyadhifa zao hadi pale kipindi cha
mpito kitakapokamilika.
“Ndugu zangu
kwa kadri hali ilivyo, katiba hii ikipita na kurudishwa bungeni kwa hatua za
mwisho ili ianze kutumika ikiwemo kutungiwa sheria mbalimbali ni wazi asilimia
90 ya wabunge wetu wa CCM, wataipitisha kwa kishindo ili wao wajipe fursa ya
kuendelea kula nchi, kitu ambacho sisi tunakipinga,” amedai.
Chanzo ni
Gazeti la Mwanahalisi.oline
No comments
Post a Comment