Zinazobamba

BREAKING NEWS,NI MGOMO MWENGINE TENA WA MABASI,KUANZA RASMI ALHAMISI,WASEMA LIWALO NA LIWE,SOMA HAPA KUJUA


WAMILIKI wa Mabasi  yaendayo mikoani nchini (TABOA) wameitangazia mgomo wa Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na nchi Kavu (SUMATRA) kuhusu nauli mpya za mabasi zilizotangazwa na Mamlaka hiyo kwa mabasi yanayoenda Masafa marefu ambazo nauli hizo zilitarajiwa kutekelezwa kwake Alhamisi ya wiki hii kwa kusema hawataruhusu mabasi yao kupakia Abiria .Anaripoti KAROLI VINSENT endelea nayo.
          
             Akitangaza Uamuzi huo wa Mgomo  leo Jijini Dar es Salaam na Katibu mkuu wa TABOA Bwana Erenea Mrutu  wakati wa Mkutano wa Dharula uliowakutani Wamiliki mbali mbali wa Mabasi wenye lengo kujadili auamuzi wa Sumatra kuhusu nauli hizo mpya pamoja na ongezeko la Ajali ambapo amesema kwa sasa TABAO wamefikia uamuzi huo kutokana na Sumatra kutofuata hali  halisi ya Garama za usafirishaji pamoja na kushuka kwa shilingi ya Tanzania pamoja na ongezeko la Mafuta kwenye Soko la Dunia ambapo inaonyesha mafuta kupanda kila kukicha.


         Pamoja na hayo amebainisha kuwa kwa Wamiliki wa Mabasi wanafanya biashara anaodai ni ya Hasara kutokana na Mafuta kuwa juu na kitendo cha wao  kuendelea kufanya biashara ya kupakia Abiria ni kufanya kazi anaodai ni ya  Hasara,ambapo anasema Jambo ambalo  Sumatra wanashindwa kulitambua na kuendelea kupunguza Nauli za Mabasi. 
        Kwa upande wao Wamiliki wa Mabasi wameitupia Lawama  SUMATRA  kwa kusema inawadharau wamiliki hao kwa kuwachukulia  watu wa kawaida.
“hatutakubali kabisa,hawa watu hawana huruma na maana mimi leo nimewekeza zaidi ya Bilioni 9 kwenye ununuzi wa magari lakini wanatupuuza na tunajua lengo la kufanya hivi tufilisike na kazi hii ili wawape watu wao kutoka China tunasema hatukubali na iyo tarehe 29 hatutoa mabasi yetu na wafanye wao kazi maana hii biashara ni hasara tu, mbona wao serikali wameshindwa wanataka na sisi kwamba tufulisike hatukubali”
 ENDELEA KUFUATILIA MTANDAO HUU UTAPATA TAARIFA KAMILI KWANI MWANDISHI WA MTANDAO HUU KAROLI VINSENT YUPO KWENYE MKUTANO HUO WA TABOA


No comments