KASHFA KWA ZITTO KABWE,ATUHUMIWA KUPORA CHAMA CHA WATU SOMA HAPA KUJUA
![]() |
Anayejiita Mwenyekiti wa ACT-Tanzania, Lucas Limbu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu |
LUCAS Kadawi Limbu,
mwenyekiti wa taifa wa chama cha siasa cha ACT-Tanzania, ameibuka na kumtuhumu
Msajili wa vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kuingilia mwenendo wa kesi
ya madai dhidi ya Zitto Kbawe na genge lake.
Aidha, Limbu anatuhumu Jaji Mutungi
kuwabeba “wahalifu waliovamia chama chake, kukibadilisha nembo, kadi na
katiba.” Anaripoti Pendo Omary … (endelea).
Limbu aliwaambia waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, kuwa kitendo cha msajili cha kuruhusu
ACT-Tanzania kubadilishwa jina, ni kuingilia uhuru wa mahakama na kutoa maamuzi
nje ya mahakama.
Anasema, “Huyu ni Jaji wa Mahakama
Kuu. Amewahi kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufaa na hakimu wa mahakama ya mkoa.
Anajua taratibu, kwamba kuna kesi mahakamani na hivyo, siyo sahihi kuupa upande
mmoja haki, wakati shauri halijaamuiriwa.”
Kauli ya Limbu imefuatia tamko la msajili la Ijumaa 24 Aprili mwaka huu,
kuwa ACT- Tanzania imeruhusiwa kubadili jina na kuwa ACT- Wazalendo.
Limbu na wenzake watatu,
waliwasilisha mahakamani 30 Januari mwaka huu, maombi ya kuitaka mahakama
kumzuia Samson Mwigamba, Prof. Kitila Mkumbo na mawakala wao, kutojihusisha na
chama hicho.
Amewatuhumu kufanya
mapinduzi ndani ya chama; kuteka chama; kubadilisha bendera, nembo na sasa jina
la chama. Kesi hiyo imepewa Na. 1 ya mwaka 2015.
Anasema, “Msajili anajua kuwa kuna
kesi iko mahakamani. Lakini yeye kwa maslahi yake binafsi, anaingilia uhuru wa
mahakama na kutoa maamuzi ya kuifuta ACT- Tanzania na kuingiza chama kingine
cha ACT – Wazalendo.”
Anasema madai kuwa Zitto na genge
lake wameteka chama chake – Alliance Change and Transparency (ACT-Tanzania) –
kinadhihirishwa na taarifa ya Jaji Mutingi kwa vyombo vya habari inayotaka ACT
– Tanzania, kurudisha cheti cha usajili walichopewa kwa jina hilo ili wapatiwe
kingine chenye jina la ACT – Wazalendo.”
Limbu amesema “Jaji Mtungi akiwa
pia ni mwanasheria aliyebobea anayafanya hayo akijua jambo lolote likiwa
mahakamani halitakiwi kufanyiwa marekebisho.
“Tayari nimeiandikia barua Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuhusu wasiwasi wangu kwamba Jaji
Mtungi anapewa rushwa ndio maana anafanya haya maamuzi kwa makusudi,” ameeleza
Limbu.
Amesema, Msajili
Msaidizi, Sisty Nyahoza alieleza gazeti la MAWIO Jumatatu iliyopita kuwa chama
kilicho kwenye orodha ya vyama hadi siku hiyo ni ACT – Tanzania.
Alipoulizwa na mwandishi wa gazeti
hilo kuwa chama cha ACT – Wazalendo kipo na kinaongozwa na Zitto Kabwe alijibu
“… sikijui chama hicho na hapa kwetu hakipo.”
Anasema, “Leo ACT ina kadi tatu
tofauti. Je, kukubali na kuruhusu mabadiliko makubwa hayo ameshaingilia hatma
ya kesi yetu. Anajua tutashidwa. Huu ni mpango mkakati ambao unafanywa na kila
mtu sasa anajua. Nina mtaka Jaji Mutungi awambie watanzania kuna nini nyuma ya
ACT – Wazalendo.”
Akizungumzia hatma ya chama
chake, Limbu amesema “ACT – Tanzania bado ipo. Ofsi ya msajili impe Kabwe
jukwaa. Asajili chama chake. Atuache na chama chetu. Huu ni uhaini.”
Chanzo ni
Gazeti la Mwanahalisi.oline
No comments
Post a Comment