Zinazobamba

KIJO BISIMBA: LIACHENI BUNGE LIJADILI KIPIGO CHA LIPUMBA....,ADAI LINAWAJIBU HUO


Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadam (LHRC) Bi Hellen Kijjo Bisimba Akifafanua jambo kuhusu  mchakato wa katiba pendekezwa ambapo amesema ni vigumu kwa mchakato huo wa kupiga kura ya maoni kama ilivyo kwa ngamia kuingia katika tundu la sindano, japo kuwa bado kuna presha ya wenye mamlaka kushinikiza kwa kura hiyo ya maoni kufanyika hiyo April 30, 
Kituo cha sheria kupitia Mkurugenzi wake wameibuka na kusema kuwa sakata la kupigwa kwa mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF linapaswa kupingwa na wadau wote na kwamba Bunge ambalo limeonesha dhamira ya dhati ya  kujadili sakata hilo, ni vyema basi Spika wa bunge akaruhusu bunge  lijadili kwani kuzuia kulizungumzia sakata hilo litajengwa taswira tofauti katika jamii
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika Kongamano lililofanyika jijini Dareslaam mapema hii leo, Mkurugenzi huyo amesema sakata hilo ni zito na watanzania wanataka kujua hasa sababu ambazo Mwenyekiti huyo tena kwa kutumia nguvu kubwa huku kukiwa na taarifa kuwa tayari alishakubali kutawanya umma wake ambao walikuwa tayari kuandamana.
Sakata hilo ambalo tokea jana huko bungeni limeonekana kuzua taswira mpya baada ya Spika kuonekana kukataa hoja binafsi iliyowasilishwa na Mbunge wa kuteuliwa na Jakaya, Mh. James Mbatia ya kutaka kujadili kipigo alichoshushiwa Ndg Lipumba

Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadam (LHRC) Bi Hellen Kijjo Bisimba Akifafanua jambo kuhusu  mchakato wa katiba pendekezwa ambapo amesema ni vigumu kwa mchakato huo wa kupiga kura ya maoni kama ilivyo kwa ngamia kuingia katika tundu la sindano, japo kuwa bado kuna presha ya wenye mamlaka kushinikiza kwa kura hiyo ya maoni kufanyika hiyo April 30, 

Mjumbe wa ilikuwa tume ya mabadi;liko ya katiba Ndg. Hamphley Polepole akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kwa nini wanaona si wakati muafa kwa kura ya maoni kupigwa hiyo April 30, Miongoni mwa sababu ambazo Polepole amezitaja ni pamoja na katiba pendekezwa kuwa ya upande mmoja, NI katiba ambayo siyo shirikishi tokea kuanzishwa kwake.
 Aidha akizungumzia dhamira ya kuitisha Kongamano la wadau mbalimbali, lilifanyika hii leo, Bisimba amesema lengo kuu ni kuangalia changamoto za upigaji wa kura ya maoni ambayo kuanzia april 30 inatarajiwa kufanyika,
Amesema wameamua kuwaita pamoja wadau hao ili kuangalia mbivu na mbichi za katiba hiyo pendekezwa ambayo wamesema imejaa mambo ambayo wananchi hawana shauku nayo na yale ya msingi yakiacha solemba
WADAU WAKIFUATILIA MJADALA AMBAO ULIKUWA UKIENDESHWA NA WATAALAM MBALIMBALI KATIKA UKUMBI WA UBUNGO PLAZA NI KUHUSU CHANGAMOTO AMBAZO ZIMO NA SABABU ZA KUKATAA KUPIGA KURA YA MAONI KWA SASA


 MWISHO


No comments