Zinazobamba

KAMBI YA LOWASSA NDANI YA CCM YAZIDI KUMEGUKA,WENGINE WACHUKUA FEDHA ZAKE TU,SOMA HAPA KUJUAZA ZAIDI

      
   BAADA  ya Edward Lowasa kupitia taarifa ya hali ya kisiasa aliyopata akiwa ziarani Mkoa wa Mara hivi karibuni kubaini kuwa kwa sasa amepoteza mvuto Kanda ya Ziwa na kwamba baadhi ya makada wake wamehama kambi, amemtuma Mwenyekiti wa Kamati ya Wezesha Lowasa Aende Ikulu, Apson Mwang'onda kwenda kuweka mambo sawa. Kwamba, Apson Mwa'onda amewasili Mjini Bukoba ambako amepanga kuanza ziara kwenye mikoa yote ya Kanda ya Ziwa kuongeza morali na kubwa zaidi kuwamwagia fedha walengwa fedha ambazo amepewa na Lowasa. 

              Apson Mwang'onda ameambatana na Francis Tupa ambaye hivi karibuni amemteua kuwa mhamasishaji wa Wastaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa ili wajiunge na Kambi ya Lowasa. Francis Tupa ni Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa ambaye nimedokezwa kuwa aliwahi kuwa Afisa Usalama wa Taifa Mkoa. Katika ziara hiyo ya kanda ya Ziwa, Apson na Tupa wameanzia Bukoba baada ya kupata taarifa kuwa baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa waliochukua shilingi laki Mbili (200,000) wameapa kusaliti kambi hiyo kwa vile Lowasa ni fisadi na afya yake ni mgogoro hali ambayo inamuondolea sifa za kugombea nafasi ya Urais.

           Wakiwa Kanda ya Ziwa, Apson na Tupa wamepanga kukutana na viongozi wa Mkoa na Wilaya wa CCM ambao ni kambi ya Lowasa ili kuwapa mikakati mipya ya kuimarisha kambi hiyo. Pia watakutana na wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa kutoka kanda hiyo ili kuboresha kiwango cha fedha baada ya kupata malalamiko kuwa laki mbili walizopata ni fedha kidogo. Kiasi cha fedha ambacho wajumbe hao watapata bado hakijabainishwa isipokuwa taarifa zilizopo ni kwamba wajumbe walioipa mgongo kambi hiyo watapewa kiasi kikubwa zaidi ya wale wanaonekana ni 'royal' kwa Lowasa. Pia Apson na Tupa wamepanga kumnyamazisha Anthony Dialo kutokana na hivi karibuni kujitokeza hadharani na kumshambulia Lowasa hali ambayo wameitafsiri kuwa ni ishara mbaya kwa Kambi ya Lowasa hasa kutokana na kwamba Dialo alikuwa kambi yao na ni mtu mwenye ushawishi mkubwa sana Kanda ya Ziwa.
 

           Katika hali ambayo inaashiria kuwa fedha ambazo amezipata kwa njia ya ufisadi anazitumia kujijenga kisiasa na hatimaye anateuliwa kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mbunge wa Monduli ambaye pia ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi, EDWARD LOWASA ameanza kugawa fedha kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama hicho. Mkakati wake umeanzia mkoani Kagera ambapo kila mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa amepata shilingi laki Mbili ( 200,000/=) na kwamba kiasi hicho cha fedha kimetengwa kwa wajumbe wote kwa wilaya zote za Tanzania.

           Kwamba, kwa Mkoa wa Kagera, Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Kagera, Mzee Ngeze amepita kila Wilaya kugawa fedha hizo ambazo zimetoka kwa Lowasa na kwamba kazi hiyo anakamilisha leo. Wakati akikabidhi fedha hizo, Mzee Ngese amewaambia wajumbe hao kuwa hiyo ni salamu kutoka kwa Rais Mtarajiwa, Edward Lowasa na kwamba ataendelea kutoa salamu zaidi kwa kadri muda wa uchaguzi utakavyokaribia. Pia amewahakikishia kuwa lengo likitimia, watarajie mambo mazuri zaidi kutoka kwa Lowasa hiyo ikiwa ni shukrani kwake baada ya kutwaa madaraka ya Urais.

             Wadau, tofauti na mbinu zilizotumika hapo awali za kufanya vikao na hatimaye kugawa fedha, Lowasa kwa sasa amebadili mbinu hiyo kwa ngazi ya wilaya kwa kuogopa kuumbuka zaidi. Kwa hali hiyo, mbinu anazotumia ni kwa mwakilishi wake kuonana na kila mjumbe na kufanya naye kikao cha falagha kumweka sawa na hatimaye kumpa kiasi hicho cha fedha. Mbinu hiyo imeanza kutumika huko Kagera na itaendelea kwa mikoa mingine.

              Baadhi ya Wajumbe waliochukua fedha hizo huko Kagera wamesema kuwa wao wanakula tu fedha za fisadi na kwamba hawapo tayari kuiangamiza nchi kwa kumchagua mtu ambaye wanajua wazi kuwa amepatikana kwa njia za kifisadi. Pia suala la afya wameligusa ambapo wamesema kuwa kuendelea kutetereka kwa afya ya mwanasiasa huyo ni kigezo tosha cha kutomudu madaraka ya rais hata kama atachaguliwa kwa njia za kifisadi.

          huo ndo uhalisia. Hakika huyu Lowasa ni mtu hatari na anajenga msingi mbaya sana wa kutafuta madaraka ambao ulikemewa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere. Kama kila mtu anayetaka madaraka sharti atumie kiasi kikubwa cha fedha, je nini hatma ya wanasiasa ambao hawajapata fedha kwa njia za kifisadi? Na je tutarajie nini kutoka kwa mtu ambaye amechaguliwa kuongoza nchi kwa njia za kifisadi? Nini mwelekeo wa taifa letu? Nini hatma ya rasilimali za nchi tulizonazo? Hakika hii ni hatari sana na Lowasa anapaswa kutafakari na kujitathmini haya anayofanya na athari zake kwa taifa.

            Mtandao huu kushirikiana na Jamii Forum  utaendelea kuwajuza kwa kadri iwezekanavyo juu ya ziara hiyo na kila kitu kitakuwa wazi kupitia mtandao huu. Hii sasa ni kufuru. Kama Lowasa anaendelea kumwaga fedha ili tu aende Ikulu ilhali nyoyo za hao wanaopewa fedha hazipo pamoja naye, hakika ni isirafu iliyopindukia. Ni wakati muafaka sasa Kwa Lowasa kujitathmini upya ili asiendelee kupoteza fedha alizopata kwa njia za kifisadi. Pia ni wakati muafaka kwa Apson na timu yake kuachana na biashara hii ambayo bila shaka inaendelea kuwadhalilisha na kushusha hadhi zao ndani ya taifa hili.

Source: Jamiiforums

Maoni 1

Bila jina alisema ...

hakuna lolote, tunahitaji evidence ya kitu mnachokiongea, watanzania wa sasa si watanzania wa miaka ya 60, wanajua, wanaelewa na kuhoji . "Kura yako ndio mabadiliko" maneno hayasaidii!