Zinazobamba

UNAFIKI MWINGINE WA JOHN SHIBUDA HUU HAPA,KANSA YA KUWASALITI UKAWA YAZIDI KUMTESA SOMA HAPA KUJUA UNAFIKI HUPI HUO

http://freemedia.co.tz/daima/wp-content/uploads/2014/08/shibuda1.jpg

           
 Pichani ni Mbunge aliyeusaliti UKAWA John Sibuda CHADEMA picha na Maktaba

WAKATI mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda (CHADEMA) akidai kuwa hajawahi kueleimishwa kuhusu kundi la UKAWA, Tanzania Daima Jumatano limebaini ni mwongo.
            Kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), linaloundwa na vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi, liliazimia kususia Bunge la Katiba kwa madai kwamba CCM imepindua maoni ya wananchi kwenye rasimu.
          Licha ya vyama hivyo kuwazuia wajumbe wake wasishiriki Bunge wala vikao vya kamati, Shibuda, Said Arfi (Mpanda Mjini) na Leticia Nyerere (Viti Maalum) wote CHADEMA, walikaidi na kuwasili mjini Dodoma kwa ajili ya kujisajili.
          Siku chache baada ya kujisajili na kuomba udhuru kwa Katibu wa Bunge, Shibuda alikwenda jimboni kwake na kuwaeleza wazee kuwa hatagombea tena ubunge kupitia CHADEMA katika uchaguzi mkuu ujao 2015.

         Na alipoulizwa kuhusu kusaliti UKAWA, Shibuda alisema kuwa yeye si sehemu ya kundi hilo na wala hajawahi kuelimishwa juu yake.
             Alisema anachokumbuka ni kwamba kupitia viongozi wa juu wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi, walikubaliana katika kikao kuwa wabunge wa vyama hivyo watoke bungeni
na kutoshiriki vikao hivyo hadi hapo rasmu iliyoletwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba itakabojadiliwa.
             “Mwislamu hawezi kutetea Uislamu kama hajui nguzo saba za Uislamu na pia huwezi kuwa Shekhe bila kupitia Madrasa na hata katika Ukristo huwezi kuutetea kama hujui Biblia na ukusoma mafundisho, na mie siwezi kuwa UKAWA wakati sijaelimishwa juu ya kundi hilo,”alisema.
              Wakati Shibuda akisema hivyo, gazeti hili limeona nyaraka za vikao vya UKAWA ambavyo vilifanyika Dodoma ukumbi wa Msekwa wakati huo Bunge la Katiba likiendelea awamu ya kwanza, ambapo mbunge huyo alishiriki na kusaini mahudhurio.
              Mathalani kwa uchache Februari 23 mwaka huu, Shibuda alihudhuria kikao cha UKAWA na kusaini orodha ya mahudhurio akiwa mjumbe wa 91kati ya 143 waliohudhuria.
                Pia Februari 27, alihudhuria na kujiorodhesha akiwa wa 38 kati ya wajumbe 97, kisha Machi 17 mwaka huu, alihudhuria kikao kingine na kujiorodhesha akiwa wa 89 kati ya 91.
                Nyaraka hizo vile vile zinaonesha Shibuda alihudhuria kikao cha Machi 23 mwaka huu, ambap alikuwa wa mwisho katika orodha ya wajumbe 89.
             Shibuda pia alihudhuria kikao cha Machi 30 mwaka huu akiwa mjumbe wa 38 katika orodha ya wajumbe 137 wa UKAWA walioshiriki.
          Gazeti hili pia limebaini kwamba hata wajumbe wengine waliosaliti msimamo wa UKAWA, Arfi na Leticia nao wamewahi kushiriki vikao hivyo kwa nyakati tofauti, kinyume na wanavyojitutumua sasa kuukana umoja huo.
            Katika kauli yake ya kutangaza kutogombe ubunge CHADEMA, Shibuda alisema amechoshwa na kauli za vitisho na kejeli dhidi yake zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa chama hicho.
              Alisema kuwa aliingia katika chama hicho kwa hiari yake baada ya kukataa dhuluma zilizokuwa zikifanywa na CCM na
hivyo kudhani ndani ya CHADEMA kuna demokrasia na ukombozi wa kweli.
            Akizungumzia tuhuma usaliti wa kuhudhuria vikao vya Bunge la katiba, Shibuda alisema kuwa hazina msingi wowote kwani hajahudhuria wala hakuchukua posho.
“Mie ni kweli nilipita Dodoma nikitokea Dar es Salaam nikiwa njiani kuja huku na nilifika ofisi za Bunge ili niweze kupatiwa fedha za matibabu kwani nasumbuliwa na mguu,”alidai
Chanzo cha habari ni Gazeti makini la Tanzania Daima.

No comments