TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI DAR--SERIKALI YAPATA DAWA YAKE SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
Na Karoli
Vinsent
KATIKA
kukabiliana na tatizo la Msongamano wa Magari Mkoani Dar es Salaam,Serikali
imesema iko mbioni kujenga Reli kutoka Ubungo jijini hapa hadi Bagamoyo Mkoani
pwani ili kupunguza tatizo hilo kubwa linalowakabili watanzania kwa sasa.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es
Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi
Dkt. Shaaban Mwinjakana wakati
wa mkutano uliowashirikisha wadau wa Masuala ya Reli kutoa nchi tofauti Duniani,
Mkutano huo uliofadhiliwa na Serikali ya Japani, ambapo Katibu huyo alisema kwa
sasa serikali imejipanga ipasavyo kuhakikisha wanaondoa kabisa Tatizo la
Msongamo wa Magari katika Jijini Dar es Salaam,
Kutokana na serikali kupanga kujenga
Reli kutoka Ubungo hadi Bagamoyo mkoani Pwan.
“Serikali imeliona tatizo hili
msongamo wa magari na sasa tumepanga kujenga Reli itakayotoka ubungo hadi Bagamoyo
na reli hii itasaidia kwa kiwango kikubwa sana kuwapunguzia adha ya wananchi
waliokuwa wanaipata,na tayari serikali katika Bajeti ya Fedha ya Mwaka
2014-2015 tumetenga fedha kwa ajiri ya upembuzi yakinifu katika mpango huu wa
Ujenzi wa reli na tunawahakikishia watanzania mradi huu utakamilika ipasavyo”alisema
Dkt Mwinjakana
Vilevile Mwinjakana alizidi kusema
Baada ya uchambuzi yakinifu Serikali itaanza Rasmi ujenzi wa Reli hiyo na
kusema Watanzania wategemee makubwa kutokana na ujenzi wa Reli hiyo,ambapo
alisema mpango wa ujenzi wa Reli ni miongoni mwa mipango ya “Big Result now”
yaani matokeo makubwa sasa.
Katika Hatua
nyingine Wizara hiyo ya Uchukuzi imesema Ujenzi wa “Terminal Three” kwenye
uwanja wa ndege wa Mwalimu Julias Nyerere utakamilika Mwakani Mwezi wa Sita na
kusema Terminal hii itaweza kupokea watu milioni sita na kupelekea uwanja huo
kuwemo katika viwanja vikubwa kabisa barani Afrika.
No comments
Post a Comment