Zinazobamba

TAMWA, WAWATAKA WATANZANIA KUWAJIBIKA KUMTETEA MTOTO, WAWATAKA WATOE TAARIFA KUHUSU VITENDO VYA KIKATILI DHIDI YA MTOTOKAIMU


KAIMU MKURUGENZI WA TAMWA, PICHA NA MAKTA

Chama cha waandishi wa habari wanawake Tamwa wametoa wito kwa watanzania kuanza kupaza sauti zao juu ya vitendo vya kikatili vinavyofanywa na watu mbalimbali dhidi ya watoto wadogo katika jamii zinazowazunguka,

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, kaimu mkurugenzi wa chama hicho cha habari, Bi. Gladness Munuo amesema hatua hiyo ya kuwataka watanzania kupaza sauti zao imekuja kufuatia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto kuendelea kuongezeka kwa kasi katika jamii ya Kitanzania,
Munuo amesema hali ilivyo sasa inatisha kwani kuna matukio mbalimbali yameripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari huku matukio mengine yakiwa bado hayajaripotiwa

Bi Munuo Ametaja baadhi ya matukio ambayo watoto wamekuwa wakitendewa kuwa ni pamoja na vipigo kupita kiasi, ndoa ya utotoni, kuchomwa moto na kutopewa matibabu wanayostahili kutoka kwa wazazi wao
Ameongeza kusema kuwa  kila mwananchi  popote pale alipo katika nchii hii anapaswa kutoa  taarifa  katika  vituo vya msaada wa kisheria , Vituo vya polisi na Tamwa pindi wanapoona mtoto anatendewa vitendo vya unyanyasaji ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa

Aidha katika Hatua nyingine Chama hicho cha waandshi wa habari Tamwa wamebainisha wazi dhamira yao ya kuwajengea uwezo wanawake wanaowania uongozi katika chaguzi zijazo na kusema kuwa wameandaa muongozo utakaowasaidia wagombea hao kujieleza vizuri na wakaeleweka katika  jamii
Munuo amesema wamejipanga kutoa miongozo kwa wagombea wa ngazi mbalimbali za uongozi ili wanawake hao wawe na uwezo wa kujieleza,katika vyombo vya habari na mikutano mbalimbali watakayohutubia
MAGARI………………………..PRESS………………..28/08/2014


No comments