Zinazobamba

SAMWEL SITTA: TUMUOGOPE KAMA UKOMA,SOMA HAPA KUJUA KWANINI




Pichani( Katikati) Ni Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samwel Sitta akihojiwa na Waandishi wa Habari picha na Maktaba.


Na Karoli Vinsent
Samwel John Sitta, Mbunge wa Urambo Mashariki, Waziri wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba hafai kuwa kiongozi katika nchi hii kutokana na Gamba alilovaa la Unafiki.
Sitta huyu ndiye alieweka mjadala huru wa kashfa ya Richmond alipokuwa spika bunge la tisa, akajenga jina la spika bora lakini akashindwa kusimamia maazimio ya bunge yaliyobaki katika 23 kwa kuwa alilotaka alilitimiza na hatimae akafunga mjadala wakati ukiwa badi unahitajika. Hatufai
                Sitta huyu amekuwa akijinadi kuwa ni mwanachama mwaminifu ndani ya CCM lakini akadiriki kuanzisha chama chake cha CCJ kinyume na katiba ya CCM ambayo anapaswa si tu kuilinda bali kuitetea kwa hali na mali na tangu tuhuma hizi ziibuliwe hakuwahi kuzijibu “Silence means YES”. Hatufai
          Sitta huyu ni Mwanachama na Waziri wa Serikali ya CCM iliyojaa Mafisadi kiasi ya kuwa hakuna aliye Msafi kati yao huku yeye anajipambanua ni mpinga Ufisadi huku akiwa anakula na kunywa meza moja na Mafisadi pasipo kuchukua hatua yoyote ya Kisayansi walau hata kujitoa ndani ya Mafisadi hao. Hatufai


          Sitta huyu ni Mwanachama na Waziri wa Serikali ya CCM iliyojaa Mafisadi kiasi ya kuwa hakuna aliye Msafi kati yao huku yeye anajipambanua ni mpinga Ufisadi huku akiwa anakula na kunywa meza moja na Mafisadi pasipo kuchukua hatua yoyote ya Kisayansi walau hata kujitoa ndani ya Mafisadi hao. Hatufai
             Sitta wakati anagombea uenyekiti Bunge Maalum la Katiba alijinadi ni mtu wa kasi na viwango huku akijaribu kujenga jina litakolombeba ili agombee urais 2015 matokeo yake amwekwa njia panda huku Chma na kule Wananchi. Anajitahidi kukisaidia chama ili kimteue kugombea wakati huo upande wa Wananchi hawataki hata kumsikia kwa kuongoza Uchakachuzi wa maoni yao na wao ndio wapiga kura. Hatufai
               Sitta ni mwanasheria anaeshindwa kutumia ujuzi wake wa kisheria katika kuongoza Bunge Maalum matokeo yake anaungana na wasiojua katika uchakachuzi wa maoni ya wananchi ya Rasimu ya pili ya Katiba kwa masilahi yake binafsi na chama chake. Hatufai
Samwel Sitta kumbuka, Wananchi hatujayaona mabadiliko ndani ya CCM sasa tunayatafuta nje ya CCM. Umeisha kisiasa na umekichimbia kaburi chama chako na 2015 tunakizika.


       .
        Lakini kwa sasa amezidi kuvaa vazi  la unafiki kutokana na kitendo chake kibaya zaidi cha kugeuza bunge la Maalum la katiba kuwa mkutano wa Chama cha Mapinduzi CCM,tena  Sitta amekuwa anapita kila Kamati kushinikiza kile anachokitaka yeye ndio kiandikwe  kwenye Katiba.
 Jinsi gani kiongozi huyo anavyonekana kukosa hata huruma kwa pesa za Watanzania ndio maana licha ya kumaliza uspika wa bunge la jamhuri 2005-2010,tangu wakati huo hadi sasa anaendelea kuishi kwenye nyumba iliyokodishwa na Serikali kwa ajili ya Makazi Maalum  spika wa Bunge.
  Nyumba hiyo iliyopo Barabara ya Buzwagi,Masaki,Dar es Salaam,ilikodishwa  na Serikali kwa ajili ya makazi ya Spika lakini bado Sitta anaendelea kukalia wakati sio Spika.
  Nyumba ambayo Sitta ameing'ang'ania imekodishwa  kwa fedha za kitanzania Milioni 15 kwa mwezi pamoja na kupata mafuta ya Gari lita 70 huku yeye sio spika,sasa jamani huyu  ndio anapiga vita mafisadi.
      Tena ukimwona mtu anaishi kwenye nyumba hii hujue hana uchungu na Fedha za Watanzania, zaidi ya kuibuka kuwanadi watu wanaosaka Urais ndani ya chama chake akiwaita ni mafisadi wakati yeye ajitaji.
  leo anaonekana wazi Jinsi alivyokuwa mrafi wa Fedha za Watanzania baada ya kuudanganya umma kwamba Katiba inapatikana kwa kusema idadi iliyopo ya Wajumbe inatosha kupata Theluthi 2 kwa madai Umoja ya Wananchi UKAWA ni idadi ndogo sana na kujinadi hawawezi kukwamisha mchakato.
  Huku kunaitwa ni Kubwabwaja kwa viongozi tuliowachagua kwa kupenda kuongea mambo ili kupata sifa tu,baada ya yeye kuongea hivyo leo ameibuka Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema na kusema bila kuwepo kwa ukawa ndani ya Bunge la Katiba hapatikani kutokana na kukosa Theluthi 2 ya wajumbe,
   Leo Sitta anawatusi ukawa kwa ajenda gani au je analidhia mapesa ya Watanzania masikini wakutupwa yanavyoteketea kwenye bunge hilo huku katiba haipatikani,leo sitta najifanya haoni jinsi watanzania wanavyokufa Hospitali kwa kukosa Huduma bora za Afya,anajifanya kiziwi kabisa Sitta kwamba asikii kelele za Watanzania wanaolalamika ugumu wa Maisha,
   Harafu anajifanya yeye ni msafi huku moyoni mwake ni mchafu,hivi watanzania wenzangu huyu ndio mwanasiasa mwadilifu?
Tafakari

5 comments

Anonymous said...

Viongozi wengi ni wanafiki na mafisadi tu, wamekalia madaraka kwa kujinufaisha wenyewe na siyo kwa faida ya wananchi na nchi yao.

Anonymous said...

We fanya yako kila mvuta kamba huwa anavutia kwake,sasa wewe ukisubiri kiongozi wa kukukomboa Tanzania hii itakula kwako.Ikiwa ufisadi upo misikitini na makanisani iweje serikalini?.Lina Mshua wako alikaaje kifala bila kutafuta chanel ambayo ingekufanya uwe unakula bata.Utaishia kuandika mada wengine wananeemeka.

uvccm said...

Hiyo ndio bongo,ukishangaa ya Sitta kuendelea kuishi nyumba ya spika basi utazimia au kufa kabisa na ya lowassa kuendelea kupewa ulinzi na marupurupu yote kama eti waziri mkuu mstaafu!!!!!!

Anonymous said...

ccm juuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

Anonymous said...

Huyu huyu Sitta ameligeuza bunge kuwa tume ya kukusanya maoni ili waendelee kukaa Dodoma kutafuna kodi za walalahoi na wavuja jasho wa nchi hii