Zinazobamba

SAKATA LA URAIA PACHA : JK ASEMA SERIKALI HAINA MALAKA YA KUTOA AMRI

IMG_9796
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete akiingia ukumbini wakati wa kongamano la Watanzania waishio Ughaibuni lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini leo Jijini Dar es Salaam. Nyuma yake ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizendo Pinda( mwenye koti la Bluu).Hassan Silayo-MAELEZO
IMG_9810(1)
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Watanzania waishio Nje ya Nchi Bw.
Emannuel Mwachulla akitoa shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa mchango wake katika masuala ya kuwadhamini watanzania waishio Ughaibuni, wakati wa kongamano la Watanzania waishio nje ya Nchi lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini leo Jijini Dar es Salaam.
IMG_9842
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizendo Pinda akiwaeleza jambo Watanzania waishio Ughaibuni wakati wa kongamano la Watanzania waishio ughaibuni lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini leo Jijini Dar es Salaam.

IMG_9895
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete akiwaeleza jambo Watanzania waishio Ughaibuni na kusisitiza kuhusu wajibu wao wa kukumbuka nyumbani na kuendelea kuchangia katika masuala la uchumi na kijamii kwa ujumla kwa ajili ya maendeleo ya nchi
IMG_9921
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizendo Pinda akimueleza jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete wakati wa kongamano la Watanzania waishio ughaibuni lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini, leo Jijini Dar es Salaam.
IMG_9926
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete akiangalia tovuti ya Umoja wa Watanzania waishio nje ya baada ya kuizindua tovuti hiyo leo jijini Dar es Salaam.
IMG_9929
Mbunge wa viti maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Leticia Nyerere (Kushoto) akiteta jambo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete wakati wa kongamano la Watanzania waishio ughaibuni lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini, leo Jijini

IMG_9940
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watanzania waishio Ughaibuni wakati wa kongamano la Watanzania waishio ughaibuni lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini, leo Jijini Dar es Salaam.

Na Joseph Ishengoma
MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema hana mamlaka ya amri kuzungumzia uraia pacha kwa sababu ni la katiba.
Rais Kikwete amesema hayo leo katika kongamano la kwanza la diaspora lililofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam. Diaspora ni lugha
inayotumika kuwatambulisha Watanzania walioko nje ya nchi wanaojiendeleza kwa njia mbalimbali ikiwemo elimu.
Kongamano hilo la siku mbili lenye lengo la kuelimishana, kubadilishana mawazo na kujadili fursa za uwekezaji, linaudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 17 duniani.
“Serikali imelisikia suala la uraia pacha, lakini ni la kikatiba sio la Rais. Katiba ndio sheria mama sisi hatuna mamlaka ya amri kulizungumzia.”
Kwa mujibu wa Rais, watanzania waliowengi uraia pacha hauwakeleketi, hivyo diaspora wanaoishi nje ndio wanaostahili kulisukuma, lakini kwa sasa sauti
yao bado haijasikika sana, badala ya kulizungumzia kwa nguvu, wanatumia muda mwingi kuzungumzia siasa za mitaani kwenye mitandao ya kijamii pindi wanapopata nafasi.
“Sauti yenu haijasikika sana, badala yake mnatumia muda mwingi kuzungumzia siasa za mitaani. Suala la uraia pacha liko mikononi mwa Bunge Maalum la Katiba. Kama katiba haijasema nyinyi ni rais, sheria ikitungwa haiwezi kuwapa uraia,” amesema. 
Kwa mujibu wa Rais, rasmu ya Katiba iliyopo inazungumzia hadhi ya Watanzania walioko nje sio uraia. “Mnachoweza kufanya ni kushawishi wabunge wa Bunge Maalum la Katiba kukubali uraia pacha kuwa ndani ya katiba na hili sio jambo haramu, zungumzeni nao serikali haina tatizo nalo iwapo Katiba itawatambua.”
Pamoja na uraia pacha, Rais amewaomba wanadiaspora kuzingatia uwekezaji ndani ya nchi ili kuleta maendeleo ya kiuchumi, kutafuta masoko ya bidhaa ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi, kuunda umoja utakaowaunganisha na kutumia teknolojia na maalifa wanayopata nje kuendeleza taifa lao.
Kauli mbiu ya kongamano hilo ni, “Nyumbani ni Nyumbani.”
Awali Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Mizengo kayanza Pinda ametaka mkutano huo kusaidia kukata kiu ya Watanzania kupata majibu ya mambo
ambayo wamekuwa wakiulizia pindi wanapokutana na viongozi mbalimbali wanchi nje ya Tanzania.

No comments