KUMEKUCHA TANZANIA---UKAWA KUBULUZWA MAHAKAMANI,WANAHARAKATI WASEMA WAMECHOKA WASEMA HAWATANII..SOMA HAPA KUJAU HALI ILIVYO
Pichani ni Viongozi wanaounda Umoja wa kutetea katiba ya Wananchi Ukawa picha na Maktaba
Pichani ni Barozi wa Amani nchini Risasi Mwaulanga akizungumza Jambo na Waandishi wa Habari picha na Maktaba
Na Karoli
Vinsent
KILE
kichoonekana Siasa za Tanzania zimefikia mahali pabaya,Baada ya leo
Wanaharakati kuibuka na kusema wanajipanga kuwabuluza wanasiasa Wanaounda Umoja
wa Kuteta katiba ya Wananchi UKAWA pamoja na makada wa Chama cha Mapindizi CCM kwenye Mahakama ya Kimataifa makosa ya
Uhalifu The Hugue iliyoko nchini Uholanzi .
Wanasiasa hao ambao ni Freeman Mbowe
Chadema,Ibrahimu Lipumba CUF,Tundu Lissu CHADEMA,Ismail JussaCUf,Capten John Komba CCM,sababu ya
kubuluzwa mahakamani kwa wanasiasa hao inatokana wao kutoa kauli walizozitoa
ambazo zinashilia uvunjifu wa Amani wa Nchi.
Akizungumzia Maamuzi hayo Leo
Jijini Dar Es Salaam mbele ya mkutano na waaandishi wa Habari, Mwenyekiti wa wa
Kamati ya Amani Tanzania,Risasi Mwaulanga,alisema kwasasa hawafanyi mzaha na
kwa sasa wako teyali wamewasiliana na Mwendesha Mastaka Mkuu Madame Fatou
Bensuda wa mahakama ya kimataifa ya Uhalifu The Hugue ili kwenda kuwashitaki wanasiasa ambao wataka kuhalibu amani ya nchi.
“Hatuwezi kuvumilia uvunjifuu huu
wa Amani ambao unataka kufanywa na hawa wanasiasa Freeman Mbowe Chadema,Ibrahimu Lipumba
CUF,Tundu Lissu CHADEMA,Ismail JussaCUf,Capten John Komba CCM,kutokana na kauli
zao za kuhalibu amani ya nchi,kwasababu ya tama zao za madaraka na sasa
tunaandaa ushahidi ili tukawashitaki kimataifa wanasiasa hawa wanafiki”alisema Mwaulanga.
Mwaulanga ambaye ni Miongoni mwa
Watanzania wapenda amani alisema sababu inayowalenga wanasiasa hawa inatokana
na baadhi ya maneno ambayo wamekuwa wakitaamka ambayo yanalenga kabisa kuvuruga
amani ya Nchi ,
Maneno hayo ni Katiba mpya
itapatikana kwa Ngumi na mateke kauli hii aliitoa Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema,kauli nyingine aliitoa Capt John Komba
aliyoisema Serikali Tatu ikipita atakwenda msituni,
Kuhusu wanasiasa wengine wakiwemo
Ibrahimu Lipumba CUF,Ismahili Jussa CUF,wanawapeleka kutokana na wao kuungana
katika kutoa matamko machafu ambayo nayo yanalenga kuchafua Amani ya nchi.

No comments
Post a Comment