MCHAKATO WA KATIBA MPYA WAITESA CCM,SASA YATUMIA MAMLUKI KUWACHAFUA UKAWA SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
| Pichani niMwenyekiti wa kamati ya Tanzania kwanza nje ya bunge AUGUSTINO MATEFU |
Na Karoli Vinsent pamoja na Exaud Mtei
Katika kile kinachoonekana ni kuanza kuchafuana kwa wanasisasa badala ya
kutafuta mwafaka wa kuwapatia watanzania katiba mpya Mwenyekiti wa kamati ya
Tanzania kwanza nje ya bunge AUGUSTINO MATEFU ameibuka mbele ya wanahabari muda
huu jijini Dar es salaam na kutoa tuhuma kali
juu viongozi wanaoongoza umoja wa
katiba Tanzania UKAWA kuwa wana msaada wa kifedha kutoka katika mataifa ya
ulaya yanayowasaidia katika kuhakikisha kuwa Mchakato wa katiba haufanikiwi.
Akizungumzan
na wanahabari leo jijini Dar es salaam mwenyekiti huyo amesema kuwa terehe 4-15
mwezi wa tatu mwaka huu UKAWA kupitia account ya kiongozi wao FREMAN MBOWE
ziliingizwa kiasi cha shilingi za kitanzania billion 1.7 kupitia moja ya benk
kubwa jijini uholanzi kupitia taasisi moja kubwa inayojihusiaha na ufadhili wa
asasi za kiraia nchini humo kwa ajili ya kusaidia katika harakati za kukwamisha
mchakato wa katiba nchini Tanzania.
Akizungumza
bila kuwa na ushahidi wowote wa jina la account,wala ushahidi unaoweza
kumwaminisha mtanzania amesema kuwa pia mnamo terehe 26,march 2014 UKAWA pia
walipokea kiasi sh 380,000,000 kupitia account ya MBOWE kutoka moja ya benk
kubwa na maarufu nchini ujerumani tawi la berlin aliyepokea pesa hizo ni
mwenyekiti MBOWE na aliyekuwa anajua ni ndugu DK SLAA NA MBOWE pekee,na wengine
kama pr LIPUMBA,MBATIA hawajui kutumia ndio maana prf lipumba alidai hazijui fedha hizo.
Aidha katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amesema
kuwa juzi mbowe alipokea kiasi cha shilingi 580,000,000 kwa lengo la kufadhili
maandamano ambayo amedai yaiweka nchi hatarini hivyo TANZANIA KWANZA inatoa rai
kwa wazalendo kutounga mkono mipango hiyo ya kuchafua amani ya Tanzania
iliyodumu kwa miaka 50
Mtandao huu ulipotaka kujua juu ya undani wa tuhuma hizo mwenyekiti huyo
ameonekana wazi kuwa hana ushahidi wa kina juu ya hilo kwani hata tulipotaka
kupata jina la hizo ACCOUNT ili kujiridhisha kabla ya kuwaeleza watanzania
alidai kwa sasa hana majina wala namba za hiyo account jambo ambalo liliwapa
wasiwasi waandishi waliokuwa wanamsikiliza.
No comments
Post a Comment