MAJI YAFIKA SHINGONI! TFF KUREJESHA OFISI ZAKE KARUME.SOMA HAPA KUJUA
Na
Boniface Wambura, Dar es salaam
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeamua kurejesha ofisi zake Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume kwa vile mipango ya uendelezaji wa eneo hilo bado
haijakwenda kama ilivyopangwa awali.
Uamuzi
huo ni moja ya maazimio yaliyofikiwa kati ya Kamati ya Utendaji ya TFF na
ujumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) uliokuwepo nchini
kwa wiki nzima kwa ajili ya kufanya mapitio (review) ya uendeshaji wa TFF.
Akizungumza
Dar es Salaam leo (Agosti 17 mwaka huu), kiongozi wa ujumbe huo wa FIFA
uliokuwa na maofisa sita, Zelkifli Ngoufonja amesema wamepitia maeneo
mbalimbali ya uendeshaji wa TFF na mpira wa miguu kwa ujumla na kukubaliana
kufanya uboreshaji kwa lengo la kuongeza ufanisi
No comments
Post a Comment