Zinazobamba

TAWLA YAZINDUA HUDUMA YA SIMU BILA MALIPO, LENGO NI KUWASAIDIA WANANCHI WENGI MSAADA WA KISHERIA


Mwenyekiti wa TAWLA Aisha Zumo Bade, akifafanua juu ya huduma ya simu bila malipo iliyozinduliwa hii leo makao makuu ya chama hicho jiji Daresalaam, Katika uzinduzi huo Madam Bade amewahakikishia wananchi kuwa huduma hiyo sio moto wa kivuu wa kuanza kwa kasi na kuzimika kwa kasi badala yake huduma hiyo itakuwa endelevu ili iweze kutimiliza malengo ya kuwapatia wateja wake msaada wa Kisheria.

Mwenyekiti akitoa ufafanuzi kuhusu huduma hiyo mpya iliyozinduliwa mapema hii leo, Madam Bade amebainisha mafanikio ambayo mpaka sasa chama hicho inajivunia kuwa ni pamoja na kuweza kuhudumia wateja 40,000 tokea kuanzishwa kwake chama hicho miaka 24 iliyopita. Hata hivyo amekiri kuwepo changamoto katika utoaji wa huduma hizo ikiwamo ukosefu wa fedha za kuendeshea huduma hiyo

Madam martina akisikiliza simu ya bure iliyopigwa na mmoja wa wananchi waliokuwa wakihitaji msaada wa kisheria wakati wanazindua huduma hiyo mapema hii leo. Tawla wametoa namba za kupiga simu ambazo ni 0800 75 1010 ikiwa ni simu ya mkononi  pamoja na ile ya mezani ya 0800 11 00 17

Hapa madam Bade alipokutana na waandishi wa habari mapema hii leo, Bade amewataka wanawake walio katika mazingira magumu watumie fulsa hiyo waliyopewa kutoa malalamiko yao ili haki yao ya msingi iweze kupatikana. Tumejikita katika kuhakikisha haki inapatikana kwa wateja wetu tena kwa wakati hivyo wateja wetu hususani wale waliokatika mazingira magum tumieni mwanya huu kutafuta haki zenu mlizokuwa mnaminya kwa muda mrefu sana,

No comments