Zinazobamba

TAARIFA KUHUSU MATOKEO YA MITIHANI YA UALIMU ILIYOFANYIKA MEI 2014, SOMA HAPA KUPATA UFAFANUZI WA MATOKEO YA UALIMU 20132014







TAREHE 16 JULAI, 2014
TAARIFA KUHUSU MATOKEO YA MITIHANI YA UALIMU
ILIYOFANYIKA MEI 2014

  1. UTANGULIZI

Baraza la Mitihani la Tanzania katika kikao chake cha 100 kilichofanyika tarehe 15 Julai, 2014 liliidhinisha kutangazwa rasmi matokeo ya Mitihani ifuatayo iliyofanyika Mei 2014:

    1. Mtihani wa Ualimu Daraja la A (Grade A Teacher’s Certificate Examination – GATCE);

    1. Mtihani wa Stashahada ya Ualimu Sekondari (Diploma in Secondary Education Examination – DSEE); na

    1. Mtihani wa Stashahada ya Ualimu Ufundi (Diploma in Technical Education Examination – DTEE).


  1. USAJILI, MAHUDHURIO NA MATOKEO YA JUMLA

    1. Usajili na Mahudhurio

      1. Mtihani wa Ualimu Daraja A - GATCE

Watahiniwa waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Ualimu Daraja A ni 10,827. Wasichana walikuwa ni 4,093 sawa na asilimia 37.80 na wavulana ni 6,734 sawa na asilimia 62.20 ya watahiniwa wote waliosajiliwa.

Kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa 10,789 walifanya Mtihani, wakiwemo wasichana 4,078 (99.63%) na wavulana 6,711 (99.66%).

Watahiniwa 38 (0.35%) hawakufanya Mtihani, kati yao wasichana ni 15 (0.37%) na wavulana ni 23 (0.34%).

      1. Mtihani wa Stashahada ya Ualimu Sekondari - DSEE

Watahiniwa waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Stashahada ya Ualimu Sekondari ni 4,931. Wasichana walikuwa ni 1,698 sawa na asilimia 34.44 na wavulana ni 3,233 sawa na asilimia 65.56 ya watahiniwa wote waliosajiliwa.

Kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa 4,899 walifanya Mtihani ambapo watahiniwa 1,685 (99.23%) ni wasichana na wavulana walikuwa 3,214 (99.41%).

Watahiniwa 32 (0.65%) hawakufanya Mtihani wakiwemo wasichana 13 (0.77%) na wavulana 19 (0.59%).

      1. Mtihani wa  Stashahada ya Ualimu Ufundi - DTEE

Watahiniwa waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Cheti cha Ualimu Ufundi ni 03 ambapo wote watatu (3) walikuwa wavulana na wote walifanya Mtihani huo.

      1. Muhtasari wa Usajili na Mahudhurio

Watahiniwa waliosajiliwa, waliofanya na wasiofanya Mitihani ya Mei 2014 ni kama inavyooneshwa katika jedwali lifuatalo:


AINA YA MTIHANI
VITUO
JINSI
WALIOSAJILIWA
WALIOFANYA
WASIOFANYA
No
%
No
%
Grade A Teacher Certificate Examination (GATCE)
94
F
4,093
4,078
99.63
15
0.37
M
6,734
6,711
99.66
23
0.34
T
10,827
10,789
99.65
38
0.35
Diploma In Secondary Education Examination (DSEE)
52
F
1,698
1,685
99.23
13
0.77
M
3,233
3,214
99.41
19
0.59
T
4,931
4,899
99.35
32
0.65
Diploma In Technical Education Examination (DTEE)
1
F
0
0
0
0
0.00
M
3
3
100
0
0.00
T
3
3
100
0
0.00


  1. MATOKEO YA MTIHANI
    1. Mtihani wa Ualimu Daraja A (GATCE)

Jumla ya watahiniwa 10,695 sawa na asilimia 99.62 ya waliofanya Mtihani wa Ualimu Daraja la A mwaka 2014 wamefaulu. Kati ya watahiniwa hao, wasichana ni 4,049 sawa na asilimia 99.66 na wavulana 6,646 sawa na asilimia 99.60.

Mchanganuo wa ufaulu kwa kila Daraja ni kama ifuatavyo :

DARAJA LA UFAULU
WAVULANA
WASICHANA
JUMLA
IDADI
ASILIMIA
IDADI
ASILIMIA
IDADI
ASILIMIA
Distinction
0
0.00
0
0.00
0
0.00
Credit
1,454
21.79
844
20.77
2,298
21.40
Pass
5,192
77.81
3,205
78.88
8,397
78.21
Supp.
6
0.09
7
0.17
13
0.12
Fail
21
0.31
7
0.17
28
0.26







    1. Mtihani wa Stashahada ya Ualimu  Sekondari (DSEE)

Jumla ya watahiniwa 4,161 sawa na asilimia 85.71 ya waliofanya Mtihani wa Stashahada ya Ualimu mwaka 2014 wamefaulu. Kati ya watahiniwa hao, wasichana ni 1,401 sawa na asilimia 83.64 na wavulana 2,760 sawa na asilimia 86.79.

Mchanganuo wa ufaulu kwa kila Daraja ni kama ifuatavyo :

DARAJA LA UFAULU
WAVULANA
WASICHANA
JUMLA
IDADI
ASILIMIA
IDADI
ASILIMIA
IDADI
ASILIMIA
Distinction
0
0.00
0
0.00
0
0.00
Credit
4
0.13
1
0.06
5
0.10
Pass
2,756
86.67
1,400
83.58
4,156
85.60
Supp.
397
12.48
261
15.58
658
13.55
Fail
23
0.83
13
0.92
36
0.86


    1. Mtihani wa Diploma ya Ualimu Ufundi (DTE)

Watahiniwa wote watatu (3) waliofanya Mtihani wa Stashahada ya Ualimu Ufundi wameshindwa baadhi ya masomo, hivyo watarudia masomo waliyoshindwa katika Mtihani wa Mei 2015.

    1. Muhtasari wa matokeo yote

Muhtasari wa matokeo ya mitihani yote iliyofanyika Mei 2014 ni kama inavyooneshwa katika jedwali lifuatalo:

AINA YA MTIHANI
JINSI
WALIOFANYA
WALIOFAULU
WANAORUDIA
WALIOSHINDWA
No
%
No
%
No
%
GATCE
KE
4,078
4,049
99.66
7
0.17
7
0.17
ME
6,711
6,646
99.60
6
0.09
21
0.31
JML
10,789
10,695
99.62
13
0.12
28
0.26
DSEE
KE
1,685
1,401
83.64
261
15.58
13
0.78
ME
3,214
2,760
86.79
397
12.48
23
0.72
JML
4,899
4,161
85.71
658
13.55
36
0.74
DTEE
KE
0
0
0.00
0
0.00
0
0.00
ME
3
0
0.00
3
100
0
0.00
JML
3
0
0.00
3
100
0
0.00

  1. MATOKEO YALIYOZUIWA

Baraza la Mitihani limezuia matokeo ya mtihani ya watahiniwa 95 ambao walifanya mtihani bila kulipa ada. Kati ya watahiniwa hao, 51 ni wa GATCE na 44 wa DSEE. Matokeo ya watahiniwa hawa yatatolewa mara baada ya watahiniwa kulipa ada wanayodaiwa.

  1. MATOKEO YALIYOFUTWA
Baraza la Mitihani limefuta matokeo ya mtahiniwa mmoja (01) wa GATCE aliyebainika kufanya udanganyifu wakati wa Mtihani.

Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuchukua fursa hii kuzipongeza Kamati za Uendeshaji Mitihani za Mikoa na Wilaya, Wakuu wa Vyuo na Wasimamizi wa Mitihani ya Ualimu iliyofanyika Mei, 2014 kwa kuzingatia na kusimamia taratibu za Uendeshaji Mitihani vizuri na hivyo kuzuia udanganyifu kufanyika. Aidha, Baraza linawapongeza wahitimu wa kozi za Ualimu kwa kutojihusiha na udanganyifu wakati wa kufanyika kwa mitihani hiyo.

  1. UPATIKANAJI WA MATOKEO YA MITIHANI YA MEI 2014

Matokeo ya Mitihani ya Mei 2014 yanapatikana katika Tovuti zifuatazo:





Dkt. Charles E. Msonde
KAIMU KATIBU MTENDAJI
16/07/2014

Hakuna maoni