RUGIMBANA AZINDUA VITAMBULISHO KWA WAKAZI WA KINONDONI
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana leo amezindua rasmi utoaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi Wilaya ya Kinondoni, na kuwa mtu wa kwanza kupokea kitambulisho chake mbali na kuwakabidhi wananchi 22 Vitambulisho vyao kutoka Kata ya Saranga mtaa wa Matangini.
Hapa anamkabidhi mmoja wa wananchi
Bi. Chiku Issa Waziri kitambulisho cha Taifa, akishuhudiwa na Maafisa
Usajili katika Wilaya Bw. Dickson Mbanga Weiss na Bw. Abdulrahman Muya
Mkuu wa Wilala ya Kinondoni
akiwasili leo katika Kata ya Saranga Mbezi tayari kuzindua zoezi la
utoaji Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Kata ya Saranga, Mbezi
Dar-es-salaam
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan
Rugimbana akikabidhiwa Kitambulisho chake na Afisa Usajili Wilaya ya
Kinondoni Ndugu Abdulrahman Muya baada ya kukamilisha hatua za mwisho za
uhakiki leo Kata ya Saranga Mbezi Dar-es-salaam. Kushoto ni Bw. Dickson
Mbanga Weiss Afisa Usajili Kinondoni.
Mmoja wa wananchi wa Kata ya
Saranga akiongozwa na Afisa Usajili wa NIDA kukamilisha hatua za mwisho
za kuhakiki taarifa zake kabla ya kukabidhiwa kitambulisho chake leo,
Kata ya Saranga Mbezi.




No comments
Post a Comment