CHUO CHA USAFIRISHAJI KUAZIMISHA MIAKA AROBAINI YA UANZISHWAJI WAKE, WALIOSOMA CHUONI HAPO ENZI HIZO SASA KUKUTANA
Mkuu wa chuo cha Taifa cha usafirishaji
Dk Zakaria Mganilwa ametangaza rasmi maadhimisho ya miaka arobani ya
uanzishwaji wa chuo hicho ambapo katika maadhimisho hayo watu
mbalimbali watahudhuria wakiwepo wanafunzi waliowahi kusoma katika
chuo hicho tokea kuanzishwa kwake,
Akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho
mapema hii leo wakati akimuapisha rais mteule mpya wa awamu ya 30,
Mh. Damian Sanya, Mkuu huyo wa chuo amesema chuo kwa sasa kipo katika
maandalizi kabambe ya kufanikisha sherehe hizo muhumu zitakazofanyika
hivi punde,
Dk Mganilwa amesema katika
kulifanikisha hilo kwa ufasaha wameamua kupanga wiki nzima iliyopewa
jina la wiki ya wana NIT ili kuwapa fulsa wanafunzi mbalimbali
waliosoma katika chuo hicho kwenda kushiriki katika midahalo ambayo
itakuwa ikiendeshwa katika wiki hiyo,
“Tutakuwa na wiki ya wana NIT
kukutana na kujadili mambo mbalimbali, ikiwamo changamoto na fulsa
zilizopo katika soko la ajira ambapo tunadhani kwa mwaliko ambao
tutautoa hivyi pumbe Wanafunzi ambao walimaliza hapa toka mika hiyo
watakuja na kutupa uzoefu wao katika sekta ya usafirishaji.”
Alisema DK Mganilwa.
Aidha katika hatua nyingine Dk Mganilwa
ametangaza zoezi la kusogezwa mbele kwa tarehe za kufanyika mahafari
ya Chuo Hicho ambapo sasa mahafari hayo yatafanyika mwaka ujayo na
sio mwezi wa kumi na moja kama ilivyozoeleka,
Akifafanua sababu za kusogezwa mbele
kwa mahafari katika chuo hicho, Dk. Mganilwa amesema ni kutokana na
matatizo ya kugongana kwa tarehe za mahafari hayo na vyuo vingine
hapa nchini,hivyo kuwa vigumu kupata wageni waalikwa tunaowakusudia
katika mustakabari wa maendeleo ya Chuo Chetu,
“Unajua chuo cha usafirishaji
kinaendana kwa karibu na vyuo kama vya DIT na Arusha Tech sasa
wenzetu huwa wanafanya mahafari yao wakati wa kupinduka mwaka, kama
vile mwezi wa pili, Nimezungumza na wakuu hawa wa vyuo na
tumekubaliana mahafari ya vyuo vyetu visiweze kugongana.
Tumekubaliana nadhani mahafari yetu yatakuwa mwezi wa pili
yatakayoenda sambamba na sherehe za miaka 40 ya chuo cha taifa cha
usafirishaji.”Alisema Dk Mganilwa
Mmoja wa watendaji wakuu wa mtandao huu akifuatilia kwa makini mkutano huo wa mkuu wa chuo na rais mteule anaeapishwa mapema hii leo. |
AFUNGUKA KUHUSU MABORESHO YAJAYO
Akizungumzia kuhusu mjanga
linalowakumba wanafunzi wa chuo hicho la kutoka mbali na kampasi
hiyo, Mganilwa amesema tatizo hilo wameliona na sasa wameamua kufanya
kufungua milango kwa sekta binafsi kuchangamkia fulsa hiyo iliyopo
ili kuweza kutatua tatizo hilo,
Tunafahamu mpaka sasa tunawafunzi zaidi
ya 3000, lakini ni wanafunzi mia nne (400) wanaofaidika na makazi ya
humu ndani huku wanafunzi 2600 wakiwa wanatoka nje ya chuo, na
tunampango wa kuongeza wanafunzi wafike elfu saba (7000) mpaka
ifikapo muhula wa 2016/2017. Bila kufanya maarifa sasa tunadhani
kutakuwa na tatizo kubwa la wanafunzi wetu kuteseka,
Sasa basi tumeamua kufanya kazi kwa
mfumo wa PPP,(private public partineship),ambapo muwekezaji aliye
tayari aje awekeze hapa , tutampa ardhi ajenge jengo kubwa kwa maana
ya mabweni yenye uwezo wa kuchukua hata wanafunzi 10,000 ili tuweze
kutatua tatizo la wanafunzi wetu kuhangaika kwa kukaa mbali na
kampasi
Hii ni biashara, Muwekezaji akiweza
kuwekeza katika mabweni tunadhani kwanza atapata faida na wakati
huohuo serikali nao wanafaidika kwani wananchi wake hawatateseka
kutoka umbali mrefu kutafuta elimu hapa NIT pili watapata mapato kwa
ada zitakazo tozwa katika mabweni hayo.
Mkuu huyo amebainisha wazi kuwa sasa
kozi za Aviation zitaanza rasmi mwaka huu,huku akiwataka wanafunzi
ambao wanahitaji kujiunga na kozi hizo basi waanze mchakato mapema
AFUNGUKA KUHUSU MGOMO WAWANAFUNZI
Dk Mganilwa akifafanua, katika hatua nyingine Mganilwa amesikitishwa na migomo inayoendeshwa huku ikiwa hakuna ulazima wa kufanya hivyo |
Akizungumzia mgomo
wa wanafunzi wa hivi Punde, Mganilwa amesema amesikitishwa sana na
hatua ambao wanafunzi walioichukua akisema hatua hiyo haikuwa mahala
pake kwani baadhi ya haki zao tayari zilikuwa katika mwenendo mzuri,
Mwenyewe enzi
zangu nilikuwa mwanaharakati mzuri sana, pale Dit na najua uchungu wa
kukosa vitu, lakini inapofika wakati katika vitu mnavyodai tayari
mmepata kimoja basi mgomo huo mnausitisha, lakini hivi sasa wanafunzi
wamekuwa hawajui maana ya mgomo,
Migomo hakika
haina maana someni vijana kwani kuendekeza migoo itawaghalimu
maishani mwenu kote, watu wanatabia ya kumfuatilia mtu tokea akiwa
chuo sasa kama unaonekana unamwenendo mbaya ujue hiyo ni shida kwako,
unadhani utaweza kujiairi???? Aliohoji Mganilwa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni