kifo cha meneja wa ewura sasa jeshi la polisi launda tume ya watu tisa kuchunguza mauaji hayo., yawataka wananchi kusubili majibu ya tume hiyo ili kubaini ukweli,
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
20/05/2014
JESHI
LA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM LAANZA UCHUNGUZI WA KINA KUHUSU SABABU ZA
KIFO CHA NDUGU JULIUS S/O NITANGA GASHAZA
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limeanza kufanya uchunguzi wa kina kuhusu
sababu za kifo cha bwana JULIUS S/O
NITANGA @ GASHAZA , miaka 51, Meneja Biashara wa EWURA, Mkazi wa YOMBO VITUKA
(Jet- Rumo). Afisa huyo alikutwa amefariki tarehe 18/05/2014, Kata ya YOMBO
VITUKA, (M) Ilala katika nyumba ya kulala wageni iitwayo MWANGA LODGE katika
chumba Na: 133 katika hali ambayo inaashiria kujinyonga kwa kutumia tai
aliyokuwa ameivaa mwenyewe.
Licha ya maelezo hayo, Jeshi
la Polisi Kanda Maalum linafanya uchunguzi ili kuondoa utata ulioanza
kujitokeza kuhusu kifo hicho hasa baada ya tarifa kuanza kuzagaa kwamba kifo chake kilitokana na kutoelewana
na viongozi wenzake katika masuala ya kikazi. Kinachofanyika ni kupata maelezo
ya kina kuhusu mwenendo wa shughuli za marehemu na hali iliyomsibu kabla ya
kifo chake kwani marehemu hakuacha ujumbe wowote aidha wa maandishi au wa
mdomo.
Aidha, Kamishna wa Polisi
Kanda Maalum Dar es Salaa ameunda jopo la wapelelezi likiongozwa na Mkuu wa
Upelelezi Kanda Maalum D’Salaam akishirikiana na wataalam wa Maabara Kuu ya
Polisi (Forensic Bureau) katika kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio
hilo. Aidha maelezo mbali mbali ya mashahidi yanaendelea kuchukuliwa ili kujua
kama kuna kosa la kijinai, kiutawala au yote.
Taarifa kamili ya mwelekeo wa shauri hili itatolewa hivi karibuni.
MAJAMBAZI
WAWILI WALIOKUWA WANATAFUTWA WAKAMATWA WAKIMILIKI BASTOLA.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
limewakamata majambazi wawili huko KIWALANI MINAZI MIREFU, (M) Ilala wakiwa na
Bastola moja aina ya STAR LANCER yenye namba SA CAL 22LR HK 708022 ikiwa na
risasi moja ndani ya Magazine. Walipohojiwa walikiri kuhusika katika matukio
kadhaa ya ujambazi na waliwataja wenzao ambao wamekuwa wakishirikiana nao
katika matukio mbalimbali.
Majambazi hao waliokamatwa
na silaha ni
·
ALLY S/O JUMA ALLY @ LIKWALE
·
CHARLES S/O CHIGANGA MALIMA @ PASTOR, miaka
32, mkazi wa Tandale Uzuri.
Aidha, watuhumiwa
waliotajwa kushirikiana na watuhumiwa hao wanasakwa kwa mbinu zote waweze
kuwaonganisha na wenzao ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
KUKAMATWA
NA MALI ISAFIRISHWAYO KWENDA NCHI JIRANI YA BURUNDIDRC PAMOJA NA WATUHUMIWA
WATATU.
Mnamo
tarehe 18/05/2014 Jeshi la Polisi Kanda Maalum lilipokea taarifa kutoka kwa msiri kuwa kuna gari lenye Na.
T.649 BAY mali ya RUOTA INVESTIMENT limepakia mali iliyokuwa inasafirishwa
kwenda nchini BUJUMBURA-BURUNDI kutoka kiwanda cha MURZAH OIL kwamba mali hiyo
inashushwa huko Sinza Afrika Sana. Polisi walichukua hatua za haraka na kufika
eneo la tukio na kukuta mali hiyo inashushwa kutoka katika lori hilo na
kupakiwa kwenye gari namba T.571 APH aina ya Honda kwa ajili ya kubeba mzigo
huo wa sabuni za unga aina ya Pulf na T-issue.
Walipohojiwa wahusika kama
mwenye mali ana taarifa juu ya kushushwa kwa mali hiyo walishindwa kutoa
maelezo yanayoeleweka. Taratibu za kisheria zilifuatwa na watuhumiwa watatu
wamekamatwa kwenye eneo la tukio ambapo walimtaja mtu mmoja aitwaye TAIRO S/O?
kuhusika na tuhuma za mizigo hiyo.
Inasemekana mali hiyo ina
thamani ya Tshs 70,000,000/=
(Shilingi Millioni Sabini) za kitanzania ambapo mali yote imeokolewa na Polisi
inamtafuta mmiliki wa mali hiyo ili kuungana nae kukamilisha upelelezi wa
shauri hilo.
Watuhumiwa waliokamatwa
kuhusiana na tukio hili ni
·
MWARABU S/O HAKIKA, Miaka 23,
Mfanyabiashara, Mkazi wa kijitonyama.
·
IDD S/O JASINA, Miaka 48, Mfanyabiashara,
Mkazi wa Kijitonyama.
·
RASHIDI S/O SAID, Miaka 17, Mkazi wa
Kijitonyama.
KUKAMATWA
KWA MAGARI SITA YA WIZI
Mnamo tarehe 05/05/2014, Kikosi Maalum cha Kuzuia na Kupambana na wizi wa magari kiliendesha
oparesheni maalum katika jiji la Mwanza kwa kushirikiana na kikosi kazi cha
Polisi Mwanza kuyatafuta magari kadhaa yaliyoibwa jijini Dar es Salaam katika
matukio tofauti na siku tofauti. Hii ni baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum
Dar es Salaam kupokea taarifa toka kwa wasamalia wema kisha kutuma kikosi hicho
kwenda jijini Mwanza.
Katika oparesheni hiyo
yalipatikana magari sita aina mbamlimbali kama ifuatavyo:
·
Tarehe 06/05/2014, huko maeneo ya Nyakato
Buzuruga ilikamatwa gari namba T.154 CRH, T/Mark II “Grande”, rangi “Pearl
White” ikiendeshwa na GEOFREY S/O ISAKA
CHABA, Miaka 45, Mfanyabiashara, Mkazi wa Nyamanoro jijini Mwanza, aliyedai
kuuziwa gari hilo na dalali YUSUFU S/O CHACHA, mkazi wa Mwanza. Gari hili
inasemekana ni mali ya AIDA D/O AUGUSTINO HAULE, Miaka 35, Mfanyabiashara, Mkazi wa Yombo Vituka jijini
Dar es Salaam.
·
Tarehe 07/05/2014, maeneo ya Nyakato jijini
Mwanza, ilikamatwa gari namba T.438 CKP, T/VEROSA, rangi “Pearl White”,
ikiendeshwa na SHABAN S/O SALUM MGONJA, Miaka 24, Mfanyabiashara, Mkazi wa
Nyakato Sokoni aliyedai kuuziwa gari
hilo na Mchungaji YUSUPH S/O ERNEST BUJIKU wa Kanisa la PENTEKOSTAl BUZURUGA
jijini Mwanza. Gari hili liibiwa Yombo Vituka nyumbani kwa REHEMA D/O SAIDI
ILUNGA, miaka 30, Mfanyabiashara.
·
Tarehe 08/05/2014, maeneo ya CAPRIPOINT
karibu na Hotel ya Tilapia ilikamatwa gari namba T.787 BRW, T/CARINA SI, rangi
ya Silver ikiwa imetelekezwa baada ya dereva kuona msako umekuwa mkali sana.
Upelelezi wa awali unaonyesha gari hili liibwa huko Kinondoni ambalo mmiliki wake ni AMANI S/O ABDALLAH
MLILAPI wa jijini Dar es Salaam.
·
Aidha, tarehe 11/05/2014, maeneo ya
katikati ya Jiji la Mwanza ilikamatwa gari namba T.895 CTU, T/Cresta GX 100,
rangi ya Silver, ikiendeshwa na GODWIN S/O SHARTIEL KWEKA, miaka 28, mkazi wa
Nyakato jijini Mwanza. Alieleza kuuziwa gari hilo na FIDELIS S/O LAURENCE
KIMBAGE, miaka 36, mkazi wa Nyakato – jijini Mwanza. Gari hili liibiwa maeneo
ya Kinyerezi Bonyokwa nyumbani kwa
VICTOR S/O BENSON USUMA, miaka 29, mfanyabiashara.
·
Pia, tarehe 14/05/2014, huko Mkoani Geita
kwenye machimbo ya madini ya GEITA GOLD MINE lilikamatwa gari namba T.891 BFF,
T/NOAH, Rangi Nyeupe, ikiendeshwa na VENANCE S/O BUKUKU, miaka 30,
mfanyabiashara. Gari hilo liibiwa huko YOMBO BUZA nyumbani kwa SALUM S/O
MWISHEHE KULITA, miaka 32, Afisa wa Bank ya NMB Makao Makuu.
·
Tarehe 04/05/2014 huko Morogoro, lilikamatwa
gari namba T.570 BZX, T/NOAH, rangi ya Silver, ikiendeshwa na HUSSEIN S/O ALFAN
SAID @ MASOFA, miaka35, Mfanyabiashara, mkazi wa Morogoro. Alipohojiwa alidai
kuuziwa gari hilo na dalali SIWAMBALI S/O SAID MOHAMED. Gari hilo ni mali ya
MOHAMED S/O GHALIB MWARABU, miaka 42, mkazi wa Ilala.
KUKAMATWA
KWA MALI YADHANIWAYO KUWA YA WIZI
Jeshi la Polisi Kanda
Maalum D’Salaam huko maeneo ya Tabata Matumbi limefanikiwa kukamata magari
mawili yenye Namba T.539 BEX aina ya Mitsubish Canter rangi ya blue ikiwa imebeba
mabox 180 ya misumari, na T.377 CME Toyota Noah rangi nyeupe likiwa limebeba
mabox 42 ya balbu mali idhaniwayo kuwa ya wizi pamoja na watuhumiwa 3.
Hii ni baada ya Polisi waliokuwa
doria kuyatilia mashaka magari hayo.
POLISI
WAZIDISHA MAPAMBANO DHIDI YA KERO YA FOLENI JIJINI D’SALAAM
Jeshi la Polisi Kanda
Maalum D’Salaam limeamua kutumia mbinu mbali mbali mbadala ili kupambana
kikamilifu na kero ya foleni inayowakabili madereva wa magari au vyombo vya
moto jijini D’Salaam. Mbinu hizo za
kukabiliana na foleni ni pamoja na kuongeza idadi kubwa zaidi ya askari wa
Jeshi la Polisi ambao watatanda katika barabara Kuu zinazoingiza magari mengi
katikati ya Jiji wakati wa asubuhi na hatimaye wakati wa jioni, magari hayo na
kwa wakati mmoja kutoka katikati ya jiji.
Mtandao huo mkubwa wa askari wa doria utaanza kazi kuanzia saa 10
alfajiri hadi saa 5 usiku wakati msongamano huo wa magari unapokuwa
umepungua. Askari hawa wa Usalama
Barabarani na wengine kutoka vikosi mbali mbali watafanya kazi katika mtindo wa
kupokezana (shift) ili kuleta ufanisi na ubora wa kazi. Mtindo huu utawabana watumiaji wa barabara
wenye mtindo wa kutanua ambao watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria papo
kwa papo (notification fines) au kufikishwa mahakamani bila msamaha au visingizio
vyovyote.
Aidha uwepo wa askari hao
kwa wingi barabarani utapunguza makosa ya usalama yanayofanywa kwa makusudi na
wenye magari aua pikipiki ambao wengine hawajali ishara za taa za usalama
barabarani (traffic lights), uchomekeaji usiozingatia taratibu za kiusalama, mwendo
kasi, kuongea na simu za mkononi wakati dereva akiendesha gari, kutofunga
mikanda ya dereva au abiria. Aidha zoezi
hili litaenda sambamba na ukaguzi wa uzima wa magari, kutokuwa na bima, leseni
ya barabara (Road Licence) na uchakavu wa gari au pikipiki kwa ujumla. Sambamba na zoezi hili tunaomba madereva raia
wema watakaogundua madereva wanaofanya makosa ya makusudi mbele, nyuma au
pembeni watoe taarifa Polisi kwa namba zifuatazo:-
1.0732 -928728 - USALAMA
BARABARANI KANDA MAALUM
2.0713-224848 - MKUU WA USALAMA BARABARANI KANDA
MAALUM
3.0787 – 668306 – AU
022-2138177 – KIKOSI CHA 999
NAMBA ZINGINE NI ZA WAKUU WA USALAMA BARABARANI
MIKOA YA:
4.0713 – 207090 - KINONDONI
5.0655 – 678260 - ILALA
6.0658 – 376477 - TEMEKE
Tahadhari inachukuliwa
kwamba zoezi hili lina lengo la kuboresha kazi za Polisi na kuleta huduma bora
kwa watumiaji wote wa barabara na kuondoa adha kubwa ya foleni yenye kuleta
madhara ya kiuchumi na kijamii.
S.H.
KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments
Post a Comment