Zinazobamba

BREEKING NEWZZZZ, KOVA AITISHA KIKAO CHA DHARULA CHA MAKAMANDA WOTE DAR, KISA NI PANYAROAD NA BADFACE,



                                     JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA



PRESS RELEASE
24/05/2014

POLISI KANDA MAALUM WAIMARISHA ULINZI KTK JIJI LA DAR ES SALAAM NA WAMEWADHIBITI VIBAKA  KWA JINA LA MBWA MWITI AU PANYA ROAD.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanya msako na doria katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ili kuthibiti makundi ya uhalifu wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na vijana wahuni wasio na kazi maalum maarufu kwa jina na MBWA MWITU au PANYA ROAD. Maeneo yote ambayo yametajwa kuonekana vijana hao kama vile Kigogo, Magomeni, Tabata, Manzese na maeneo ya Mbagala, wamepangwa askari wa kutosha wa doria ili kuthibiti mlipuko wowote wa vitendo vya kihuni vyenye ishara ya uhalifu vinavyoleta hofu kwa wananchi.
Kwa ujumla ni kwamba vijana hao hawana uwezo tena wa kufanya uhalifu katika makundi yao kutokana na mpango kazi uliopangwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum. Aidha tayari wameshakamatwa viongozi (Ring Leaders) sita (06) wa vikundi hivyo na majina yao ni kama ifuatavyo:
·        ATHUMAN S/O SAID, Miaka 20, Mkazi wa Kigogo.
·        JOSEPH S/O PONELA, Dereva Bodaboda, Mkazi wa Kigogo Mkwajuni.
·        CLEMENT S/O PETER, Miaka 25, Fundi Selemara, Mkazi wa Kogogo.
·        ROMAN S/O VITUS, Miaka 18, Mfanyabiashara, Mkazi wa Kigogo.
·        MWINSHEHE S/O ADAM, Miaka 37, Mkazi wa Temeke Mashine ya maji.

·        DANIEL S/O PETER, Miaka 25, Mkazi wa Yombo.
Pamoja na uthibiti wa vijana hao, umezuka mtindo wa watu ambao hawafahamiki maeneo mbalimnali ya jiji la Dar es Salaam kwa kutuma ujumbe  mfupi  au simu za mkononi wakieleza uvumi kwamba maeneo yao yamevamiwa na makundi Mbwa Mwitu au Panya Road. Mtindo huo wa uvumi umeenea sana maeneo ya Kigogo, magomeni, mansese na Tabata. Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kuwa mtindo huo ukome kwani watu hao wanasababisha hofu kwa wananchi bila sababu na Jeshi la Polisi limebaini kuwa hakuna tukio lolote ambalo limefanyika maeneo hayo au kuripotiwa kituo chochote cha Polisi katika kipindi cha wiki hii ambapo uvumi umeenea sana.
Ningependa kuwatoa hofu wananchi wa Dar es Salaam kwamba si kweli kwamba kuna tishio la vijana hao kama inavyosemekana kwani Jeshi la Polisi limejiimarisha kiulinzi na vijana hao hawana uwezo wa kufanya watakavyo kama uvumi ulivyoonezwa kimakosa.
Uchunguzi umebaini kwamba chanzo cha uvumi huu ni kwamba tarehe 18/05/2014 na 20/05/2014 palitokea mauaji ya vibaka wawili waliohusishwa na makundi haya na kwamba kulikuwa na hofu kuwa baada ya mazishi ya vijana hao  vijana wenzo wangeweza kulipiza kisasi ndio maana pakawa na uvumi  wa jumbe mbalimbali zilizoleta hofu.
Tunawaomba wananchi wawe watulivu na waendelee na shughuli zao kama kawaida na waachane na uvumi huo.


S. H. KOVA – CP
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

No comments