Habari zilizoifikia FULLHABARI BLOG muda
huu ni kuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini ambaye pia ni director
Adam Kuambiana Amefariki dunia muda mchache uliopita baada ya kuanguka
ghafla akiwa location. Chanzo makini ambacho pia ni star mkubwa wa
filamu nchini kimeitumia ujumbe SWP uliosomeka "msanii Adam Kuambiana
amefariki dunia sasa hivi, alikuwa location kaanguka ghafla, maiti ipo
hospital ya Marie Stopas, Mwenge, Dar es salaam. Mungu ailaze roho yake
mahali pema peponi. Ameen.
Enzi za uhai wake Kuambiana alianza kujipatia umaarufu baada ya kuigiza
filamu ya Fake Pastors na baada ya hapo kucheza filamu nyingi zilizompa
umaarufu kabala ya kuanza kuwa director.
Tutawaletea updates zaidi kuhusu kifo cha Kuambiana ambacho ni pigo katika tasnia ya filamu nchini.
Adam Kuambiana
Breaking News: Adam Kuambiana Afariki Dunia Ghafla Akiwa Location.maiti ipo hospitari ya maria stopas
Reviewed by Full habari Digital
on
12:44:00
Rating: 5
No comments
Post a Comment