sasa serkali yasusia wanaoishi mabondeni, yasema na wafe tu sababu wametaka wenyewe kufa, ni kutokana na mvua zinazoendelea hapa jijini
| Mkuu wa mkoa wa Daresaalam akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mapema hii leo. |
Kile kinachoonekana kama liwalo na liwe, leo hii mkuu wa mkoa wa Daresalam amtaka rasmi kuwa serikali yake haitawajibika kwa matatizo yoyote yatakayojitokeza kwa wale wananchi wanaokaa mabondeni, na zile sehemu hatarishi ambazo uwezekano wa kukubwa na mafuriko ni mkubwa na kwamba yeyeote atakayengoja mafuriko yamkute ndipo aanze kulaumu serikali,hiyo itakuwa ni kazi ure,
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Daresalam, Mkuu huyo wa Mkoa amesema hatua imekkuja kufuati wakazi wa maeneo hayo kukaidikuondoka kwa hiari na hata serikali ilipotaka kuwaondoa kinguvu bado wamekuwa wakaidi na kuamua kufngua kesi mahakamani wakiitaka mahaka kuweka hati ya zuio ili wasieze kufukuzwa katika maeneo yao,
| Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini, mkuu wa mkoa wa Daresalaam akifafanua jambo mbele yao. |
Sadiki ameongez kusema kuwa sasa hakuna msalie mtume, Tatizo lolote litakalojitokeza katika mabonde hayo watajua wenyee wapeleke wapi vilio vyao kwani sasa serikali imenawa mikono kuhusiana na kadhia hiyo
Ameongeza kusema kuwa, wananchi wafahamu kuwa serikali haina nia ya kuingilia muhimili mwingine wa serikali kwa kuwafukuza maeneo yao yanayokaa, lakini wafahamu kuwa serikali haitakuwa pamoja kwa madhala yoyote yatakayojitokeza.
| Mkuu wa mkoa wa Daresalaam akisikiliza moja ya maswali ya waandishi wa habari kuhusiana na kunawa kwa serikali kuwasaidia wakazi wa mabondeni katika mafuriko yaliyotabiriwa, |
Kama unavyojua Tayari mamlaka ya hali ya hewa imeshatoa angalizo kuhusiana na mvua zinazoendelea jiji Dresalaam , hivyo watu wa mabondeni ni vyema wakatoka wenyewe kuliko kungoja mpaka mafuriko yawafunike ndipo unakumbuka kuhama, na huko hakuna na tofauti na kukumbuka shuka wakati kumeshakucha
A idha katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa wa Daresalaam amewataka wakazi wa Daresalaam kuhudhlia katika sherehe za siku ya mwanamke ambayo itafanyika march 8 pale mwembe yanga, huku mgeni rasmi akiwa waziri wa jinsia na watoto.
Meck Sadick amesema kuhudhulia kwa wananchi ndio kufankisha kwa sherehe hizo, hivyo i vyema wakatumia muda wao kuja kusherehekea kwa pamoja siku ya mwanamke ambayo kwa mwaka uu inakaul mbiu nzuri inayochochea kuheshmiwa kwa haki za mwanamke hapa nchini
1 comment
Serikali isikwepe majukumu yake. Ni lazima uwajike kwa rescue measures kwenye majanga yyte yale. Kwa maoni yangu suluhisho la kudumu la watu wa mabondeni sio kuwahamisha, maana tumeshuhudia kwamba njia hii imeshindwa nami naungana na wananchi wa mabondeni hawapaswi kuhamishwa, Serikali inapaswa kujenga miundombinu ya kudhibiti mafuriko na kuhahkikisha watu wanaishi mabondeni lakini kwa usalama. Kuna sehemu hapa hapa dunian watu wamejenga nyumba baharini na wanaishi haaingii akilini eti njia muafaka kwa serikali ytu ni kuwahamisha watu kwenda Mabwepande, tuna watlaam wa Maji na mafuriko serikalai ijenge miundombinu na watu waendelee kuishi pale jangwani na mabonde yte ni sehemu potential sn hatuwez kupakimbia eti kwa sababu ya maji tena mvua zinazoleta mafukriko mara1 kwa mwaka, ni akili ndogo tu za viongozi wetu
Post a Comment