NAPE NNAUYE AWAVAA WANAOHOJI USHINDI WA RIDHIWANI KIKWETE,
![]() |
| Katibu mwenezi wa ccm, akifafanua jambbo katika moja ya mikutano yake na waandishi wa habari, NNauye amefunguka leo kuhusiana na maneno maneno ya chinichini yanayoendelea juu ya Ridhiwani kuchaguliwa na wanachalinze kuwa mgombea wa Ubunge jimbo la Chalinze |
Sikumoja baada ya mtoto wa raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuibuka kidedea katika kura za maoni ya kumpisha mgombea kupitia chama na Tawala,na baadhi ya wanaharakati kuanza kutupa makombora wakidai ushindi huo umelenga kumbeba mtoto huyo wa rais, Katibu mwenezi wa chama hicho Bw. nape Nnauye ameibuka na kusema wazi kuwa watu wote wanaoongelea ushindi wa Ridhiwani hawana jipya zaidi ya chuki binafsi,
Akizungumza na mwandishi mahili wa mtandao huu hivi karibuni, Nape amesema watu wote wanaozungumza vibaya juu ya ushindi wa Ridhiwani Kikwete hawana jipya na kwamba ushindi wake ni harali na umepitia taratibu zote za Chama,
"Ndugu mwandishi, wewe mwenyewe umeona kulikuwa na washindani zaidi ya sita pale lakini wananchi wameamua kumpa ridhiwani sasa haya maneno madogomadogo yanatoka wapi. Angepewa ushindi huo chumani mwake hapo kungekuwa na haja ya watu kuhoji uteuzi huo sasa kila kitu kilikuwa hadharani kwa nini kunachochoko kama hizo"Alihoji Bw. Nnauye
Nnauye ameongeza kusema kuwa, wananchi wa Chalinze wanaimani kubwa na Ridhiwani na ndio maana wakampisha kwa ushindi wa Kimbunga.
Hivi karibuni Ndg. Ridhiwani Kikwete aifanikiwa kushinda katika kura maoni ya kumpisha mgombea ubunge katika jimbo la Chalinze kwa kura 758 akiwagalagaza vilivyo kina Imaan mahuhila Madega na Ramadhani Maneno waliokuwa wanamkaribia kwa karibu

No comments
Post a Comment