WAZIRI CHARLES KITWANGA APOKEA SHEHENA YA MWISHO YA MABOMBA YA GESI
Naibu
Waziri Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Mhe. Charles Kitwanga
(wa tatu kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Menjeja wa Bandari
ya Mtwara (wa pili kutoka kushoto) Bw. Absalim Bohella. Anayefuatia ni
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Wilman Kapenjama Ndile, na uongozi wa Mkoa
mara baada ya kupokea Shehena ya mwisho ya Mabomba ya Gesi katika
bandari ya Mtwara.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Bandari ya Mtwara wakiendelea na kazi ya kupakua
shehena ya mabomba ya gesi kutoka katika meli baada ya mabomba hayo
kuwasili katika Bandari ya Mtwara.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Mhe. Charles
Kitwanga akiangalia ujenzi wa kambi za wafanyakazi katika eneo la
Madimba Mtwara. Ujenzi wa kambi hizo utakapokamilika unatarajiwa kuwa na
huduma zote za muhimu. Aidha katika eneo la hilo la Madimba panatarajiwa kujengwa mitambo ya kusafisha gesi. 
Mtaalamu wa Masuala ya Gesi na Msimamizi Mkuu wa Mitambo ya Kusafisha Gesi Mhandisi Sultan Pwaga (katikati) akimweleza jambo Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Charles Kitwanga na ujumbe wake alipotembelea eneo hilo kuangalia namna shughuli mbalimbali zinavyoendelea katika eneo hilo.

Naibu
Waziri Mhe. Charles Kitwanga (wa pili kutoka kushoto) na Mkuu wa Wilaya
ya Mtwara Mhe. Wilman Kapenjama Ndile, (wa kwanza kulia) wakipata
maelezo kutoka kwa mtaalamu Abshakim Marunda kuhusu namna kisima cha
gesi cha nchi Kavu kinavyofanya kazi. Kwa mujibu wa Maelezo ya Mjiologia
Mwandamizi wa TPDC Bw.George Ngwale hayupo pichani ameeleza kuwa, Mnazi
Bay ina jumla ya visima vitano kati ya hivyo visima vine vina gesi
inayochimbwa na kisima kimoja kikavu. Aidha gesi inayopatikana katika
eneo hili inauzwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambao wanatumia
kuzalisha umeme
No comments
Post a Comment