zitto kabwe apasua jipu, adai Lissu ni kifaranga, amtaka asikurupuke kwani mkono ni swahiba mkubwa wa Freemani Mbowe

Siku moja baada ya Mwanasheria mkuu wa chama cha Chadema kutangaza hadhali madudu aliyoyafanya alikuwa katibu mkuu wa chama hicho ndugu Zitto Kabwe, Zitto Kabwe ameibuka na kupasua siri nzito iliyokuwa ikifanywa na mwenyekiti wa chama hicho taifa, Fullhabari limebaini,
Mapema majira ya saa nane na nusu hivi katika makao makuu ya chama cha chadema, Mwanasheria mkuu wa chama alitangaza wazi mbele ya waandishi wa habari, kuwa Zitto zubeir kabwe ameshiriki katika kuuza jimbo la mpanda mashariki kwa kusema kuwa Chadema haitasimamisha mgombea hali ambayo ilimuwezesha, Mgombea wa chama cha mapinduzi kupita bila kupingwa
Lissu akaenda mbele na kusema, Zitto amehongwa magari mawili na fisadi namba sita hapa nchini Mh. Nmrodi Mkono, na kwamba watu kama hao hawastahili kuwepo katika chama, kitu ambacho kinaonyesha wazi kumkwaza alikuwa katibu msaidi wa chama hicho Ndg Zitto Kabwe,
Katika majibu yake juu ya shutuma hizo za Lissu, Kabwe hakuwa tayari kukubali kwa tuhuma hizo, badala yake alimwita mwanasheria huo ni Kifaranga amabaye hana muda wa kubishana naye na anamtaka mama wa kifaranga ndie azungumze nae, hiyo ni kutokana na ukweli kuwa Lissu hajui mengi juu ya masuala ya ndani ya chadema
Zitto anasema, mwenyekiti wa chama taifa anafahamu mengi juu ya Nimrodi mkono, hivyo amemtaka Lissu kufunga mdomo wake kwani yeye hana analohua zaidi ya kuambiwa vitu nusunusu tu na mama wa kifaranga.
Haya ndio maneno aliyozungumza Zitto katika ukurasa wake wa facebook
"Angalia Zitto Kabwe alichoandika FB"
""Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono.
Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs
40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini. Nadhani alimwambia pia
mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa
Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama
ametoa mkopo na akalipwa. Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono
alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa. Pia hakusahau kumwambia kuwa
Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu anajua kuwa gazeti la
Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka Conservative party?
Nimefanya internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu masuala
ya mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri
Mkuu Pinda.
Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni
kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia
deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke
wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas.
They must know I am not a push over. Chacha died, I won't.
Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea
mtu kidole kuhusu maadili

No comments
Post a Comment