SAKATA LA KAPUYA BADO KIGUGUMIZI, KAMANDA KINONDONI ASEMA WAANDISHI TULIENI SUALA LIKO KATIKA UCHUNGUZI MZITO>>>>>>
Na Karoli
Vinsent
Jeshi la
Polisi Kanda maalum limezidi kusuasua kumchukulia
hatu kali za kisheria ,Mbunge wa
Urambo Magharibi Juma Kapuya (CCM), anayetuhumiwa kutishia kumuua binti
anayedaiwa kumbaka na kumuambukiza virusi vya ukimwi.
| Kapuya |
Hayo yalibainika leo
Jijini Dar es salaam wakati kamisha wa polisi Kanda ya Dar es Salaam, CP Suleiman
Kova wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake,ambapo waandishi wa Habari
walipokuwa wanataka kujua kwanini kunasuasua katika sakata la mbunge huyo.
Ndipo kova alionyesha
kustuka na kuanza kueleza jeshi hilo alijapata hati ya mshataka,iliyofunguliwa
polisi ndipo waandishi wa habari wakamwambia mbona taarifa hiyo imesharipotiwa
polisi kwenye kituo cha polisi cha ostabei jijini hapa ,ndipo kamisha Kova
akawataka waandishi wa habari waende kwa kamanda wa polisi wa kinondoni
Camillius Wambura kupata taarifa ya mwendelezo wa jalada la kapuya
Mwandishi wa Blogs hii
akamtafuta kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius
Wambura akasema sakata liko kwenye uchunguzi.
“sakata hilo la Kapuya
liko kwenye uchunguzi na siwezi kuzungumzia suala hilo maana lipo kwenye uchunguzi na sasa tunawasiliana na ofisi ya Dpp pindi litakapukuwa tayali hatma
hitajulikana’alisema Wambura
Mwandishi wa “blogs” hii
alipomuuliza,kuhusu kutishiwa Maisha binti huyo mwenye miaka kumi na sita na
mtu anaemiliki namba ya 0784993930 ambayo inasemekana ni ya Mbunge huyo
ambapo insemekana na inamilikiwa na Kapuya,
kamanda Wambula alisema yeye hawezi
kulizungumzia suala hilo kwani mwandishi wa blogs hii huwezo wake wa uchunguzi
ni mdogo kuliko jeshi la polisi
“Mimi siwezi kulizungumzia
suala hilo kwani wewe uwezo wako wa uchunguzi ni mdogo kuliko jeshi la
polisi,maana kuhusu nani anaemiliki namba ya simu ziko mamlaka zinazohusika
zinazohusika ndizo zinahusika”alizidi
kufafanua Wambura
Uchunguzi ulifanywa na mwandishi
wa Blogs umebaini kusuasua katika sakata
hilo,huku kuwepo na ushahidi wa wazi juu ya kitendo cha kutishiwa maisha binti
huyo na mbunge huyo kutoka kwenye simu ya mbunge huyo kwenda kwa mwanafunzi
huyo.
Ujumbe huo ambao mwandishi
wa “Blogs” alishuhudia Moja ya ujumbe wa
vitisho unaodaiwa kutumwa na Kapuya kupitia simu hiyo unasomeka hivi: “Mkiuawa
itakuwa vizuri…itawapunguzia gharama za kuishi, usitake kugombana na serikali
mtoto mdogo kama wewe, sisi ndiyo wenye nchi yetu, mwenye hilo gazeti ni Mbowe,
sasa mwambieni nyumba ya kuishi si mmemuingizia hela leo
“Mnatumika
tu bure watu wanaingiza hela nyingi, ila mmenitibua lazima niwaue wiki hii
haitaisha, nitapiga kambi kote, jana si wamekuficha tuone utalindwa milele
maana washatengeneza hela, lazima mvae sanda tu hilo sio ombi ni wajibu wenu,
mnajitia na nyie mafia watoto siyo, watoto wetu wanauza unga nani anawakamata?
Nani atapingana nasi.”
Mwandishi wa mtandao huu
alishuhudia jalada la kesi hiyo lenye jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo
cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam ambapo mwandishi wa mtandao
huu alishudia lakini bado mpaka sasa mbunge huyo hajachukilwa hatua
No comments
Post a Comment