NINAPOTAFAKARI KUHUSU MAFANIKIO HAYA, >>>> HAKIKA MGANILWA UNAPASWA KUPONGEZWA
![]() |
| MKUU WA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI AKISALIMIANA WACHEZAJI WANAFUNZI, MGANILA AMESEMA CHUO HICHO SASA KUWA KIMBILIO LA WATU |
Mkuu wa chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT) Eng Zakaria Mganilwa amewataka vijana kuchangamkia fulsa zinazojitokeza katika chuo hicho kama kweli wanataka kuongeza uwanja wa soko lao la ajira katika nchi hii,
Eng Mganilwa ameyasema hayo mapema hii leo wakati akizungumza na Wanafunzi wa chuo hicho jinsi chuo hicho kilivyojipanga kuhakikisha wanatoa elimu bora inayokidhi matakwa ya soko,
Mganilwa amesema kwa sasa chuo kinampango kabambe wa miaka mitano ulioanzia 2011/2012-2015/16 ambao katika mpango huo chuo kinatekeleza mipango mbalimbali ya kujijenga chuo pamoja na kukitambulisha chuo kimataifa,
Akizungumzia miongoni mwa mambo yanayotekelezwa katika mpango makakati huo wa miaka mitano, Mganilwa ameendelea kufafanua kuwa ni pamoja kuongeza courses 6 mwaka 2005 hadi kufikia takribani kozi 27 kwa mwaka 2013 katika chuo hicho
UJENZI WA KITUO CHA UKAGUZI WA MAGARI
Akizungumzia kuhusu ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa magari katika kampasi hiyo ya chuo, Mganilwa amesema tayari zoezi la ujenzi wa kituo hicho kinakwenda vizuri na mpaka sasa kituo hicho kipo katika hatua za mwisho na kwamba wanatarajia mambo yakienda vizuri, mwanzoni mwa Januari wana kutumia kituo hicho kukagulia magari hapa nchini,
Mkuu huo amefafanua kuwa tayari chuo kimeshapata kazi ya kukagua magari toka TBS na kinachosubiriwa kwa sasa ni umaliziwaji wa kituo hicho na kazi ya ukaguzi ianze mara moja
"Zamani serikali ilikuwa inakagua magari kwa kupitia mawakala wake kulekule yanakotengenezwa magari lakini kulikuwa na baadhi ya matatizo yalijitokeza sasa Tbs imetupa kazi ya kukagua magari yote yanayoingia nchini ambako mawakala hawapo" aliongeza Eng Mganilwa
Aidha, Mganilwa ameongeza kusema kuwa kwa sasa chuo kiko katika mazungumzo na jeshi la polisi ili kuweza kuona ni namna gani magali yote kabla hayajapewa leseni na mamlaka ya SUMATRA,
Amesema hali ilivyo sasa ni kwamba jeshi la polisi ndilo lenye dhamana ya kukagua magali na baada ya hapo Sumatra watoa leseni kwa gari hizo kufanya biashara yake, lakini tunaona ni vema tukapewa kazi hiyo kutokana na ukweli kuwa sisis tuna dhana za kukagulia hayo magali na kuweza kugundua kama yanapaswa kuwa barabarani au laa
Kama mitambo tunayo, kama nguvu kazi tunayo, nadhani tuna kila sababu ya kupewa kazi ya kukagua magari yote hapa nchini, kabla hayajapewa leseni na sumatra, hii itaboresha kwa kiasi kikubwa ufanisi wa magari yatakayotembea katika barabara zetu,
Kwanza wenzetu wa polisi wanafanya visual inspection unakwenda polisi kwa kupeleka kadi ya gari tuu kisha unaandikiwa katika kadi yako kama umefanyia ukaguzi tayari kwa kwenda kupewa leseni ya biashara, hiyo haitoshi tunazani kunahaja ya kwenda mbele na kukagua magali yenyewe,
Nadhani kwa kufanya hivyo kwa kiasi fulani tunapunguza magari kuuu barabarani, na kupunguza ajali za barabarani,
Aidha katika hatua nyingine mkuu huyo amewataka wanafunzi na wananchi kwa ujumla kuanza kuchangamkia mafaunzo ya ukaguzi magari, iliyoanzishwa hapo chuoni ili waweze kuongeza uwanja wao wa soko la ajira,
Kwa sasa taifa linampango la kuanzishwa vituo vya kukagua magari nchi nzima, na wafanyakazi wa sekta hiyo watatoka NIT nawaombeni jifungeni mkanda mchangamkie fulsa hii muhimu, msiache nyuma Aliongeza Eng Mganilwa,
UKAMILISHWAJI WA NATIONAL TRANSPORT RESOURCE CENTER
Kuhusu kukamilika kwa jengo kuu linalotarajia kuwa kitovu cha kupata taarifa zote zinahusu sekta ya usafirishaji, Mganilwa amesema, jengo hilo liko katika hatua nzuri, na mwakani litaanza kutumika rasmi,
Amesema kumalizika kwa jengo hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi wa chuo hicho kujisomea katika mazingira yaliyo bora zaidi, na kwamba wanatarajia itakuwa chachu ya kuongeza wanafunzi wengi mwakani kutokana na kukamilika kwa jengo hilo,
![]() |
| MOJA YA VITI AMBAVYO MGANILWA AMENUNUA KATIKA UTAWALA WAKE |
Amesema chuo tayari kimeshanunua jumla ya viti 1000 na madawati 1000 tayari kwa kuanzia masomo kwa mwaka ujao katika jengo hilo,na pia amebainisha wazi kuwa wanategemea jumla ya wafanyakazi wapya 50 wanatarajiwa kujiunga na timu ya wataaramu wa nit mapema wiki ijayo ili kuendelea kutoa elimu iliyo bora hapa chuoni,
Ameongeza kusema kuwa, kukamilika kwa jengo hilo ni faraja kwa taifa kwa ujumla hii ni kutokana na ukweli kuwa taarifa zote muhimu zinahusu sekta ya usafirishaji sasa zitapatikana katika kituo cha National transport resource center (NTRC) hapa NIT
Taarifa muhimu kama, ajali za barabarani, magari yanayoingia nchini na yalisajiriwa, na taarifa zinazofanana na hizo, ambazo hapo awali ilikuwa ni lazima uzitafute katika Wizara mbalimbali kama, wizara ya mambo ya ndani, na wizara ya fedha kwa taarifa kama, ajali za barabarani, usajiri wa magari, na viwango vya ubora wa magari .
NIT SASA KUUNGANISHWA NA MKONGO WA TAIFA
Habari njema kwa wanafunzi wa national institute of transport na wale wanaotaka kujiunga na chuo hicho ni kwamba kwa sasa chuo kipo katika hatua nzuri ya kuunganishwa na mkongo wa taifa, hatua inayotarajia kuongeza kasi ya kutafuta material on line
Akizungumza katika kikao maalum na wanafunzi wa chuo hicho, mkuu huyo wa chuo amebainisha wazi kuwa kwa sasa waziri wa mawasiliano, amemuhakikishia wazi kuwa chuo hicho kitaingia katika mkongo wa taifa.
Akizungumzia faida za kuunganishwa katika mkongo huo wa taifa, Mganilwa amesema itasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kutafuta material kama ya CILT ambayo tumefulsa ya kutembelea on line lakini mpaka sasa tunashindwa kufanya hivyo kutokana na kasi ya internet kuwa chini,
AANZISHA BAJETI YA KUKARABATI CHUO KWA KILA MWAKA
Katika kuhakikisha kuwa chuo kinakuwa katika mandhari ya kurizisha, chuo kimeandaa utaratibu kutenga fedha za kukarabati chuo hicho mipango mingine itakayoifanya jumuiya ya wana nit kuishi katika chuo hicho kwa amani na bila kupata shida ya maji, umeme na shida zinazolingana na hizo
Amesema kila mwaka wanatarajia kutenga jumla ya shilingi MILIONI 200-300 ili kukabiliana na matatizo ya namna hiyo


No comments
Post a Comment