Zinazobamba

KWA TAARIFA YENU SISI TUKO HURU, MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI NEC AFUNGUKA

JAJI DAMIAN LUBUVA AKIFAFANUA JAMBO KWA MWANDISHI WA HABARI HIZI KUHUSU UHURU AMBAO TUME YAKE INAYO, JAJI ALISISITIZA KUWA TUME YAKE IKO HURU NA HAKUNA KUBANWABANWA NA WAKUBWA
 Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Nec  mapema hii leo ameibuka na kusema kuwa  tume yake iko huru na kwamba hakuna dalili zozote zinazoonyesha kuwa tume yake inabanwa katika kutekeleza majukumu yake ya kila leo

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwakwe, Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Damian Lubuva  amewataka watanzania kufahamau kuwa tume yake iko huru na kwamba anawataka waiamini kutokana na ukweli kuwa tume yake imedhamilia kuleta imaani ndani ya watanzania,

WAANDISHI WAKIFUATILIA KWA MAKINI UFAFANUZI WA jAJI LUBUVA, TUME IKO HURU JAMANI, TUPENI USHIRIKIANO TUFANYE KAZI
Timu hiyo mpya ambayo imeingia madarakani kwa takribani miaka miwili iliyopita imefikia hatua baada ya kuwa na tetesi kuwa mwenyekiti wake, kwa maana ya Jaji Lubuva ametamka rasmi kuwa tume yake inafanya kazi kwa kubanwabanwa kwa maana siyo tume huru hivyo kudhua maswali mengi kwa wananchi uharali wa kufanya kazi katika tume hiyo kama haina uhuru wa kutosha,

Jaji lubuva ameongeza kusema kuwa tumeyake, iko huru na ameendelea kuyasema hayo hata katika mikutano mbalimbali alikarishwa, ikiwamo ile ya chuo kikuu cha Daresalaam, Chuo cha Iringa Na hata Nairobi ambapo alienda katika mijadala mbalimbali

Amesema watanzania wengi wamekuwa wakisema kuwa Tume yake hako huru kutokana na qwafanyakazi wa tume hiyo wengi wao wanaazimwa toka serikalini, hatua inayosadikiwa kuwa wanaweza kufanya kazi ya kupendelea chama tawala hivyo vyama pinzani  kuwa na nafasi finyu ya kushinda chaguzi




No comments