MKAKATI WA KANDA WABAINIKA, NI ULE WA KUTAKA KULETA SERA ZA KIKANDA, WATAKA KUMSIMIKA MAGUFULI KUWA RAIS WA AWAMU YA TANO >>>>, SOMA HAPA
NA Karoli
Vinsent
BAADHI ya viongozi wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Kanda ya Ziwa, wameandaa mkakati kuhakikisha Rais katika
Uchaguzi Mkuu wa 2015, anatoka katika kanda hiyo, huku zikielezwa sababu nne
zilizowasukuma kuwa na mtazamo huo wa kikanda.
BAADHI ya viongozi wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Kanda ya Ziwa, wameandaa mkakati kuhakikisha Rais katika
Uchaguzi Mkuu wa 2015, anatoka katika kanda hiyo, huku zikielezwa sababu nne
zilizowasukuma kuwa na mtazamo huo wa kikanda.
Mgombea anadaiwa kuwa Waziri wa
Ujenzi, Dk. John Magufuli, ambaye ni kutoka Kanda ya Ziwa. Magufuli anadaiwa na
wafuasi wake hao kuwa amejizolea umaarufu miongoni mwa wananchi kutokana na
utendaji wake wa kazi na wapo wanaodai amekubali kuwania nafasi hiyo ingawa bado
hajaweka hadharani.
Taarifa zaidi ambazo bado
hazijathibitishwa na Waziri Magufuli zinadai kwamba amekubaliana na masharti ya
kundi hilo la kikanda.
Hata hivyo, kundi hilo limepata pigo
baada ya aliyekuwa mwenyekiti wake katika kuratibu na kuwaweka pamoja wadau
muhimu wa kundi hilo, Clement Mabina, kuuawa na wananchi wenye hasira mwanzoni
mwa wiki iliyopita.
Katika kikao kilichofanyika kwenye
moja ya hoteli zilizoko eneo la Capripoint jijini Mwanza asubuhi ya siku ya
maziko ya aliyekuwa diwani wa Kisesa na Mwenyekiti wa zamani wa CCM, Mkoa wa
Mwanza, Clement Mabina, kilichowakutanisha mawaziri Samuel Sitta, Steven
Wassira na John Magufuli, mikakati mipya ya kuendeleza harakati hizo baada ya
Mabina kuuawa, iliazimiwa.
Mabina aliteuliwa kushika nafasi hiyo
ya uratibu kwa sababu mbalimbali, moja ikiwa ni kutokuwa na uongozi katika
chama na hivyo kumuwezesha kufanya mizunguko bila ya kushtukiwa au kusababisha
maswali kutoka kwa viongozi wa juu wa chama.
Katika kutekeleza mkakati huo,
baadhi ya viongozi wa Kanda ya Ziwa ambao tayari walikuwa wakionyesha nia ya
kuwania urais mwaka 2015, wamefikiwa na kamati hiyo iliyokuwa ikiongozwa na
Mabina, ikielezwa kwamba wengi walikubali kumuunga mkono mgombea wao.
“Waziri Steven Wassira ni kweli
alitangaza nia kwa wajumbe wa NEC mkoani kwake na alianza kupata uungwaji mkono
katika baadhi ya mikoa na hata huko Zanzibar, lakini walimfuata na kumweleza
kwa nguvu yake pekee, hawezi kumudu na ana vikwazo vingi kwa hiyo wakamwomba
awaunge mkono na amekubali wako pamoja,” kilidai chanzo chetu cha habari kutoka
ndani ya kamati hiyo ya uratibu.
Wassira anadaiwa kukatishwa tamaa
kuendelea na dhamira yake hiyo kwa sababu zinazodaiwa kuwa ni kutokuwa na
vigezo vya kumudu nguvu ya upinzani, hasa kwa kuwa alikwipata kuwa mpinzani na
kukisema vibaya Chama cha Mapinduzi kwa wananchi.
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na
Madini, William Ngeleja naye anadaiwa kujiunga katika harakati hizo na hata
kuahirisha harakati zake za awali za kutaka kuwania nafasi hiyo kwa msukumo
wake binafsi.
Kambi hiyo ambayo imepata uungwaji
mkono mpaka katika mikoa ya Tabora na Kigoma ambako wanasiasa machachari wa
mikoa hiyo wamekubali kuiungana mkono ili kudhibiti kasi ya kundi lolote
wanalodhani ni tishio dhidi ya malengo yao.
Moja ya sababu ya kupata nguvu kwa
kambi hiyo ya Kanda ya Ziwa inatajwa kuwa ni kutokana na minyukano ya kisiasa
ndani ya CCM, kiasi kwamba baadhi ya makada wake hawako tayari kuona kundi
jingine likifanikiwa na hivyo kuwa tayari kuungana na kundi lolote lile
ilimradi linaweza kukwamisha juhudi za kundi jingine.
Mbinu zinazotumiwa na kundi hilo kwa
sasa ni kwa baadhi ya wafuasi wa kambi hiyo kutangaza kuwania nafasi ya urais
na kuanza harakati za kuomba kura kwa wajumbe wa NEC na mkutano mkuu, lakini
nyuma ya mkakati huo yupo mgombea maalumu wa kanda hiyo, ambaye anatakiwa
lakini amezuiliwa asizungumzie masuala hayo ili atakapojitokeza wakati muafaka
kuwe na nguvu kubwa na mvuto.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa kanda
hiyo iko katika mazungumzo ya kuungana na wenzao wa Nyanda za Juu Kusini ili
wawe na nguvu ya pamoja katika kuamua nani anakuwa mgombea wa CCM katika
Uchaguzi Mkuu ujao.
“Lakini pia wana mpango mbadala,
kama ikifika hatua mgombea wao anashindwa kupenya wataingia katika makubaliano
na kanda anakotoka mgombea mwenye nguvu, ili aweze kubeba agenda zao na tayari
yako mazungumzo na kanda ya Nyanda ya Juu Kusini na yanaendelea vizuri,”
kinaeleza chanzo chetu cha habari ndani ya kamati hiyo ya urais wa kikanda.
Kanda ya Ziwa ambayo inatajwa kuwa
na turufu muhimu ya kuamua mshindi katika vikao vya chama kutokana na idadi ya
wajumbe wake, wameibua mambo manne ambayo wanataka kuyasimamisi kikamilifu.
Mambo hayo ni pamoja na kuwa na chuo
kikuu cha umma katika Kanda ya Ziwa, kuifanya Mwanza mji muhimu kiuchumi katika
ukanda wa maziwa makuu hasa katika kuboresha uwanja wake wa ndege na kuwa na
nafasi muhimu katika vyombo vya uamuzi, ikiwamo Kamati Kuu ya CCM.
Tafsiri kadhaa zimekuwa zikijitokeza
kuhusu waliohudhuria maziko ya Mabina hivi karibuni. Miongoni mwa waliohudhuria
maziko hayo ni Waziri Magufuli, Waziri Stephen Wassira, Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais – Mazingira, Charles Kitwanga.
Wachambuzi
wa Masuala ya kisiasa nchini wliozungumza na Mwandishi wa mtandao huu wanasema
kitendo cha viongozi wa kanda ya ziwa kujipanga kuteua mgombea wa Urais kutoka
huko kunaweza kuleta migongano mikubwa ndani ya chama cha CCM na kupelekea
mpasuko ndani ya chama,
Mpasuko,huu
utatokea endapo Nguvu kubwa anayotumia Waziri mkuu aliyejiuzuru na pia ni
Mbunge wa Munduli Edward Lowasa katika kutaka urais kwani malazote amekuwa na
nguvu kubwa ndani ya chama pamoja na nje ya chama kitendo cha kanda ya ziwa
kuteua mgombea wao kunaweza kuleta mpasuko.
Kutokana na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli kuwa na Upenzi kwa
wananchi kutokana na uwajibikaji wake kwa wananchi na kama Kanda ya ziwa
wakimsimamisha Magufuli basi Halamshauri kuu ya Chama hicho inawakati mgumu
sana katika kupendekeza jina la mtu hatakayechukua nafasi ya urais, .
Duru za
kisiasa zinasema kisiasa zinasema Chama cha Mapinduzi CCM kitaingia kwenye
mpasuko mkubwa endapo Jina la Edward Lowasa kama litakatwa kutokana na kuweka
jina la mtu mwengine.
No comments
Post a Comment