Kenya yaadhimisha miaka 50 tangu ipate uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza
![]() |
| Wanafunzi nchini Kenya wakipeperushe bendera kusherekea uhuru wa nchi hiyo, katika maadhimisho ya mwaka uliopita Photo: AP |
Na Flora Martin Mwano
Wananchi wa Kenya wameadhimisha miaka hamsini ya Uhuru katika sherehe
zilizoongozwa na rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta jijini Nairobi na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika wakiwemo marais
na Mawaziri Wakuu. Maelfu ya watu wameshiriki maadhimisho hayo
yaliyofanyika katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi na kuanza kwa
burudani kutoka makundi mbalimbali.
Miongoni mwa marais waliohudhria maadhimisho hayo ni pamoja na Goodluck
Jonathan wa Nigeria, Joyce Banda wa Malawi, Joseph Kabila wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya congo, Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, Yoweri
Museveni wa Uganda na wengineo wengi.
Katiba hotuba yake kwa taifa rais Uhuru Kenyatta ameleezea mafanikio ya
kichumi, kisiasa, kielimu na mambo mengine yaliyopatikana kwa kipindi
cha miaka 50 iliyopita.
Akizungumza na maelfu ya wakenya katika maadhimisho hayo, rais wa
Tanzania Jakaya Kikwete ameipongeza Kenya kwa kupiga hatua kubwa katika
nyanja mbalimbali na kusisitiza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na
Kenya katika miaka ijayo kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo
mawili na kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Naye rais wa Uganda Yoweri Museveni alitumia nafasi hiyo kuyakosoa
mataifa ya Magharibi kukataa kusitisha kesi inayomkabili rais Uhuru
Kenyatta na naibu wake William Ruto katika Mahakama ya Kimataufa ya ICC
na kusema kuwa bara la Afrika litaendelea kupigania haki zake.
Marais wengine waliozungumza katika maadhimisho hayo na kuwapongeza
wakenya katika miaka 50 ya Uhuru wao ni pamoja na Joyce Banda wa Malawi,
Ali Bongo Ondimba wa Gabon na Goodluck Jonathan.
Kenya inaadhimisha miaka 50 ya uhuru ikiwa imepiga hatua kubwa ya kuwa
na uchumi imara miongoni mwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki licha ya
kukabiliwa na changamoto mbalimbali.
Kenya ilipata uhuru wake tarehe 12 Desemba,1963, kutoka kwa Muingereza
baada ya harakati za mapambano ya kundi la Mau Mau zilizoanza katika
miaka ya 1950.

No comments
Post a Comment