HEBU SOMA WARAKA HUU WA TUNDULISU, KWA WANAMABADILIKO
Wanamabadiliko,
Nina mambo mawili. Moja, kwa kadri mjadala huu ulivyo hadi sasa,
inaelekea kuwa kila mmoja wetu anaamini kwamba ni kweli huyu bwana
kafanyiwa fujo Kama anavyodai. Hii assumption kwamba anachosema kweli
kimetokea haina msingi wowote zaidi ya maneno yake mwenyewe. Hajatoa
ushahidi wowote kuthibitisha madai yake. Hajataja jina la Mhusika hata
mmoja aliyeshiriki kumfanyia fujo. Mwanasheria wa BAVICHA could be me, I
was there na nadhani huyu bwana ananifahamu, Kama sio kwa jina angalau
kwa sura. Ameulizwa Kama ametoa taarifa polisi, inaelekea hajatoa.
Lakini hata Kama angekuwa ametoa would it necessarily be true kwamba
amefanyiwa fujo? Si itakuwa ni tuhuma tu zinazohitaji uthibitisho?
Kinachonisumbua ni hicho kwamba badala ya kumhoji juu ya ukweli wa
maneno yake tunayajadili as if yamethibitishwa kwamba ni ya kweli.
Pili, it seems to me hadithi hii, pamoja na mapungufu yake mengi,
ina lengo moja tu: kuichafua na kuipaka matope CHADEMA. Choice ya
kichwa cha habari 'NIMEFANYIWA FUJO KONGAMANO LA UHURU CHADEMA' ni ya
makusudi na ina lengo hilo. Swali kama waliomfanyia fujo, kama ni kweli,
wametumwa na viongozi au la ni la makusudi na lengo ni hilo hilo.
Tatu, kama nadharia yangu ni ya kweli kwamba hadithi hii lengo ni
kuichafua CHADEMA na viongozi wake, then haitakiwi kutustaajabisha hata
kidogo. Huu ni mwendelezo wa vita ya ugaidi dhidi ya Wilfred Lwakatare,
Henry Kilewo na wenzao na CHADEMA iliyoanza mwaka jana na kuisha
katikati ya mwaka huu Mahakama Kuu Dar na Tabora. Mshiriki Mkuu (MM?) wa
vita hii alikuwa Mwigulu Nchemba, Dennis Msaki, MM mwingine wa majuzi
na mapolisi akina Advocate Nyombi na kundi lao!
Kwa wasiokumbuka naomba nirudie kilichotokea. Kwa zaidi ya mwezi mzima
kabla ya tarehe 28 Desemba, Ludovick alikuwa akiwasiliana na Dennis
Msaki kwa simu kuliko alivyokuwa akiwasiliana na mke wake wa ndoa. Siku
ya tarehe 28 Desemba (wakati au kabla au baada ya kumrekodi Lwakatare
kwa Siri) aliwasiliana kwa simu na Mwigulu Nchemba. Kesho yake tarehe 29
asubuhi Mwigulu Nchemba, MM na Julius Mtatiro wa CUF walionekana kwenye
Star TV ambapo Mwigulu Nchemba alidai kuwa na ushahidi wa video wa
viongozi wa CHADEMA wakipanga mauaji ya waandishi habari. MM
hakumkanusha! Tarehe 14 Januari 2013 Mwigulu Nchemba alimtumia Ludovick
sh. 50,000 kwa M-Pesa.
Baadae video ya ugaidi wa CHADEMA ilipowekwa kwenye YouTube na Lwakatare
kukamatwa, MM alikuwa kiongozi pekee wa CHADEMA aliyeandika kwenye
mtandao hadharani kwamba Lwakatare asimamishwe uongozi ili achunguzwe
kuhusiana na njama hizi za kigaidi. The message was loud and clear:
CHADEMA should distance itself from it's security chief ili anyung'unywe
peke yake bila msaada halafu akipatikana na hatia, iwe ni hatia ya
chama pia! Ni bahati mbaya tu kwamba mipango hii ilishindwa baada ya
chama hiki chenye watu wenye 'akili ndogo' na 'elimu ya magumashi'
walidaka ushahidi wote huu na kupambana na wajanja na wasomi hawa
hadharani!
Ludovick na wanaomtumia walishindwa Mara ya kwanza. Wanafikiri watashinda Mara ya pili. Tusubiri!

No comments
Post a Comment