1000 wakisiwa kuuwawa Sudan Kusini, ni katika vita kati ya majeshi ya Salva Kir na na ya makamu wa rais wa zamani wa nchi hiyo Bw.Riak Machar
![]() |
Mapigano makali yanaendelea
Sudan Kusini, baina ya wanajeshi wa serikali ya Rais Salva Kiir, na wale
watiifu kwa makamo wa rais wa zamani, Riak Machar.
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa, Hilde Johnson, anasema watu zaidi ya elfu moja wameuwawa, ingawa idadi hasa haijulikani.Ripoti zinasema viongozi hao wamejadili juu ya uwezekano wa kusitisha mapigano, mazungumzo ya kutafuta amani, na maafa ya raia hivi sasa.
Haijulikani kama viongozi wa Ethiopia na Kenya watakutana na Bwana Riek Machar piya.
Mwandishi wa BBC mjini Nairobi anaeleza kuwa Sudan Kusini ni muhimu kibiashara kwa jirani zake.
Kenya imeiuzia nchi hiyo bidhaa za thamani ya dola 290 milioni mwaka huu.
Serikali ya Kenya inasema raia wake kama 1,000 bado wamenasa katika miji ya Sudan Kusini - wafanya-biashara, walimu, wafanyakazi katika usalama na wachuuzi.
Piya kuna wasiwasi kuwa mapigano yakizidi yataakhirisha ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ya Sudan Kusini hadi bandari ya Lamu, Kenya.

No comments
Post a Comment